Pata taarifa kuu
Venezuela

Sherehe za kuapishwa kwa Hugo Chavez zasogezwa mbele

Serikali ya Venezuela imethibitisha kuwa itasogeza mbele sherehe za kuapishwa kwa rais Hugo Chavez ambaye kutokana na matatizo ya kiafya aatashindwa kuhudhuria sherehe hizo zilizokuwa zimepangwa kufanyika hapo kesho.

Rais wa Venezuela, Hugo Chavez
Rais wa Venezuela, Hugo Chavez
Matangazo ya kibiashara

Makamu wa rais Nicolas Maduro ameliambia bunge la nchi hiyo kuwa kamanda Chavez ameomba kusogezwa mbele kwa sherehe hizo kutokana na ushauri aliopewa na madaktari wanaomtibu.

Upinzani nchini humo umetaka rais Chavez akabidhi madaraka yake kwa makamu wake na kuongeza kuwa kutofanyika kwa sherehe hizo ni kinyume cha katiba ya nchi.

Hapo kesho maelfu ya wafuasi wa kiongozi huyo wamepanga kufanya maandamano makubwa kumuunga mkono rais Hugo Chavez.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.