Pata taarifa kuu
Venezuela

Malumbano ya Kikatiba kati ya Upinzani na Serikali ya Venezuela yashika kasi

Malumbano ya kikatiba yanaendelea kushika kasi nchini Venezuela huku Serikali ikitoa wito kwa Raia kujitokeza kumuunga mkono Rais wa Taifa hilo, Hugo Chavez kabla ya kuapishwa kwake kwa ajili ya kutumikia Muhula mpya.

Rais wa Venezuela, Hugo Chavez
Rais wa Venezuela, Hugo Chavez REUTERS/Jorge Silva
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Habari nchini humo, Ernesto Villegas hapo jana alisema kuwa hali ya Chavez inaenddelea kuimarika tangu alipopata tatizo baada ya kufanyiwa upasuaji wa awamu ya nne.
 

Hatua ya kutaka kuungwa mkono kwa Rais Chavez imekuja baada ya kuwepo kwa Malumbano juu ya uwezo wa Serikali ya Chavez kuendelea kubaki mamlakani iwapo Chavez afya yake itaendelea kudorora.
 

Kiongozi wa upinzani wa juu nchini Venezuela, ameitisha maandamano ikiwa Serikali ya nchi hiyo itachelewesha shughuli za kuapishwa kwa Rais wa Taifa hilo Hugo Chavez ambaye hali yake yaelezwa kukutereka baada ya kufanyiwa upasuaji kwa awamu ya nne.
 

Kiongozi huyo wa Upinzani Julio Borges pia ameahidi kufungua kesi ya malalamiko ikiwa tarehe 10 ya mwezi Januari iliyopangwa kuapishwa kwa Rais haitatekelezwa.
Upinzani umedai kuwa Mamlaka ya Venezuela inapindisha katiba kutokana na matatizo ya Chavez.
 

Upinzani umefikia hatua hiyo imefikiwa wakati kukiwa na taarifa kuwa huenda Chavez asiapishwe siku ya Alhamisi kufuatia hali yake kuwa tete.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.