Pata taarifa kuu
MEXICO

Polisi nchini Mexico wamkamata kiongozi wa juu wa kundi la Zetas linalojihusisha na biashara ya dawa za kulevya

Jeshi maalumu la wanamaji nchini Mexico limetangaza kufanikiwa kumkamata kiongozi wa juu wa kundi Zetas linalojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya  nchini humo.

Polisi maalumu wa Mexico wakiwa wamewakamata watuhumiwa wa biashara za dawa za kulevya
Polisi maalumu wa Mexico wakiwa wamewakamata watuhumiwa wa biashara za dawa za kulevya Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hao wamesema kuwa walimkamata Ivan Velazquez kiongozi wa juu wa kundi la Zetas kwenye mji wa San Luis Potosi na kuongeza kuwa kukamatwa kwake kumetokana na mgawanyiko ambao umeanza kujitokeza ndani ya makundi ya uuzaji dawa za kulevya nchini humo.

Ivan anatajwa kuwa miongoni mwa viongozi wa juu wa kundi hilo ambao walikuwa wanasakwa na Serikali kwa muda mrefu kwa tuhuma za kushiriki mauaji ya raia wasio na hatia mjini Mexico.

Kukamatwa kwa kiongozi huyo kumeonekana kuwa ni mafanikio kwenye operesheni iliyoanzishwa na rais Felipe Calderon ambaye ameapa Serikali yake kukabiliana na makundi makubwa ya uuzaji dawa za kulevya nchini humo.

Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kuonyeshwa mbele ya waandishi wa habari katika tukio ambalo linasubiriwa kufanyika muda wowote kuanzia sasa ambapo wananchi watapata nafasi ya kumshuhudia kiongozi huyo.

Ivan ambaye hufahamika pia kwa jina la El Taliban amekuwa mmoja wa waasisi wa kundi la zetas lilioanza kujipatia umaarufu nchini humo kwenye miaka ya 1990 ambapo limekuwa likifanya biashara ya uuzaji dawa za kulevya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.