Pata taarifa kuu
MEXICO

Jeshi la polisi Mexico lafanya mabadiliko kukabiliana na biashara ya dawa za kulevya

Wizara ya mambo ya ndani nchini Mexico hapo jana imewahamisha askari wake wote waliokuwa wanalinda doria kwenye uwanja wa ndege wa kimatiafa wa Benito Juarez na kupeleka askari wapya baada ya kutokea mashambulizi ya risasi kati yao.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya wizara hiyo imesema kuwa zaidi ya askari 348 wamehamishwa kwenye uwanja huo.

Baada ya kuhamishwa hivi sasa wamepelekwa askari wapya kutokana na hivi karibuni kuuawa kwa maofisa kadhaa wa polisi kufuatia walinzi hao kugeukana kwa sababu za biashara ya dawa haramu za kulevya.

Licha ya Juhudi za serikali kukabiliana na makundi ya wauzaji wa dawa za Kuelvya nchini humo, polisi imeelezwa kukithiri kuwa na viongozi wanaoshirikiana na makundi hayo.

Nchi ya Mexico inatambulika kama kinara wa biashara haramu ya dawa a kulevya biashara ambazo kila kukicha zinapigwa maarufuku na nchi mbalimbali duniani licha kuendelea kushamiri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.