Pata taarifa kuu
MAREKANI

Siasa za Republican zapamba moto, Mitt Rommney ashinda majimbo matatu

Mitt Romney ambaye anasaka kuteuliwa kuwa Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Republican nchini Marekani ameendelea kujihakikisha nafasi hiyo baada ya kushinda kwenye majimbo mengine matatu ambayo ni Washington, Maryland na Wisconsin.

REUTERS/Darren Hauck
Matangazo ya kibiashara

Ushindi wa Romney unamsogeza katika kinyang'anyiro cha Urais dhidi ya Mgombea wa Chama Cha Democratic Rais Barack Obama kwenye uchaguzi ambao unatarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Rick Santorum na Newt Gingrich hawakuambulia kitu mbele ya Romney ambaye kwa sasa anatajwa kuwa na nguvu kuwa kwani ameweza kuungwa mkono na wajumbe wengine na hapa hakukosa neno baada ya ushindi huo.

Romney baada ya kupata ushindi huo ameendelea kukosoa utawala wa Barack Obama kuwa umeshindwa kutekeleza yale yaliyotarajiwa na wapiga kura.

Amesema akipata nafasi ya kupambana na Barack Obama ana uwezo wa kumshinda na kuwa rais ambaye ataleta mabadiliko makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.