Pata taarifa kuu
NEW YORK-MAREKANI

Polisi mjini New York wafanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa ugaidi

Jeshi la Polisi katika Jiji la New York nchini Marekani linamshikilia Jose Pimentel mwenye umri wa miaka ishirini na saba kwa kosa la ugaidi baada ya kubainika kupanga na kutekeleza shambulizi la bomu kulenga magari ya polisi na ofisi za posta.

REUTERS / Andrew Burton
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Polisi linamshikilia kijana huyo ambaye anaaminika kuwa na uhusiano wa karibu na Mtandao wa Al Qaeda baada ya kutekeleza mashambulizi kulenga maeneo mbalimbali ya Jiji la New York.

Meya wa New York Michael Bloomberg akiwa na Kamanda wa Polisi wa Jiji hilo Raymond Kelly wamewathibitishia waandishi wa habari kukamtwa kwa Pimentel na sasa yupo chini ya ulinzi.

Kufuatia kukamatwa kwa kijana huyo polisi mjini New York wameendelea kuimarisha usalama katika jiji hilo kufuatia hofu ya kutekelezwa kwa mashambulio ya kigaidi toka kwa watu wanaodhaniwa kuwa wanashirikiana na kijana huyo.

Polisi wamesema kuwa kuwa wamefanikiwa kunasa maandiko ambayo Pimentel aliyaandika yanayoonyesha kupanga njama za kutaka kuwauwa askari na wahudumu ambao wanatokea nchini Iraq na Afghanistan ambako walikuwa wanatumikia majeshi ya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.