Pata taarifa kuu
ARGENTINA

Mahakama Nchini Argentina imemhukumu adhabu ya kifungo cha maisha Mwanajeshi wa zamani

Mahakama Nchini Argentina imemhukumu adhabu ya kifungo cha maisha Afisa wa zamani wa Jeshi la Majini nchini humo Alfredo Astiz ambaye alikuwa anatambulika kwa jina la utani la Malaika wa Kifo kutokana na kumkuta na hatia ya mauaji na kukiuka haki za binadamu wakati wa utawala wa Kidikteta.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Astiz mwenye umri wa miaka hamsini na tisa amekutwa na hatia ya makosa hayo pamoja na ukatili ambayo aliyafanya wakati wa Utawala wa Kidikteta uliohudumu katika nchi hiyo tangu mwaka elfu moja mia kenda sabini na sita hadi elfu moja mia tisa themanini na tatu.

Makosa hayo yalifanyika wakati mwanajeshi huyo akifanyakazi chini ya Utawala wa Kijeshi ambao unatajwa ulijaa ukatili na kutenda dhulma kubwa kwa wananchi ambao walilazimika hata kukimbia nchi hiyo.

Hukumu ya kesi hii inakuja wakati hapo awali Mashirika ya Kimataifa ya Kutetea Haki za Binadamu yakitaka Astiz pamoja na wanajeshi wenzake wa zamani kumi na wawili waliohusika kwenye kutekeleza ukiukwaji wa haki zabinadamu wachukuliwe hatua za kisheria.

Astiz alishawahi kuhukumiwa kifungo cha maisha jela na Mahakama moja nchini Ufaransa licha ya mwenyewe kutokuwepo mahakamani hayo baada ya kukabiliwa na kosa la mauji ya Alice Domon na Leonie Duquete yaliyotekelezwa mwaka elfu moja mia tisa sabini na saba.

Lakini hukumu hiyo ambayo imetolewa na Mahakama ya Argentina imejumuisha makosa ya kuuawa kwa wanawake hao wawili wa Ufaransa, Mwandshi wa Habari Radolfo Walsh pamoja na makosa mengine ya mauaji ya ukatili dhidi ya raia.

Taarifa ambazo zimetolewa na Mamlaka nchini Argentina zinaeleza kuwa zaidi ya watu elfu tisa walitekwanyara wakati wa Utawala huo wa Kidikteta huku watu wanaofikia elfu thelathini wakiuawa wakati huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.