Pata taarifa kuu
MAREKANI

Utata waibuka kuhusu kesi ya Dominique Strauss-kahn

Kesi ya kashfa ya ngono inayomkabili mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Fedha Duniani IMF, Dominique Strauss-Kahn imechukua sura moya baada ya kuibuka kwa taarifa kuwa mshtaki ametoa maelezo ya uongo kwa polisi.

Reuters/Allan Tannenbaum
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hizo ambazo zimepatikana toka kwa wanasheria kadhaa wa marekani zinasema kuwa kumebainika kuwa mwanamke ambaye anamshtaki Strauss-Kahn, amekuwa akitoa maelezo tofauti pindi alipohojiwa kwa nyakati tofauti na polisi kuhusiana na kesi aliyofungua.

Raia huyo wa Marekani mwenye asili ya nchini Guinea alimshtaki Strauss-Kahn katika mahakama ya mjini New York akidai kuwa alizalilishwa kijinsia na bosi huyo wa zamani wa IMF.

Kwa nyakati tofauti, wanasheria hao wamesema kuwa kumebainika kuwepo kwa maelezo tofauti toka kwa mshtaki baada ya kuhojiwa na polisi ambapo amekuwa akitoa maelezo yanayokinzana kuhusiana na kesi hiyo.

Taarifa kutoka nchini humo zinasema kuwa mwanamke huyo aliyemshtaki Strauss-Kahn pia amebainika ana kesi nyingi polisi zinazomuhusisha yeye na matumizi ya dawa za kulevya na hivyo polisi kuangalia uwezekano wa kufuta mashtaka yanayomkabili.

Sakatia la kutolewa kwa maelezo feki na mshtaki huyo linakuja ikiwa muda mchache ujao Dominique Strauss-Kahn anatarajiwa kupandishwa kizimbani ambapo wanasheria wake wanatarajia kuwasilisha maombi mapya ya kulegezwa kwa masharti ya dhamana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.