Pata taarifa kuu

Niger: Maandamano dhidi ya uwepo wa jeshi la Marekani yafanyika

Maandamano dhidi ya uwepo wa jeshi la Marekani, nchini Niger yamefanyika. Mashirika ya kiraia yalitoa wito kwa raia kuingia mitaani kutaka kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani nchini humo. Maelfu ya watu walikusanyika katika mji mkuu kuunga mkono serikali ya Baraza la Kitaifa la Ulinzi wa Nchi (CNSP) ambayo inaimarisha ushirikiano wake na Urusi.

[Picha ya zamani] Katika picha hii iliyopigwa Aprili 16, 2018, bendera za Marekani na Niger zikipandishwa bega kwa bega katika kambi ya wanajeshi wa anga na wafanyakazi wengine katika kambi ya 201 ya jeshi la wanamaji huko Agadez. (Picha ya kielelezo)
[Picha ya zamani] Katika picha hii iliyopigwa Aprili 16, 2018, bendera za Marekani na Niger zikipandishwa bega kwa bega katika kambi ya wanajeshi wa anga na wafanyakazi wengine katika kambi ya 201 ya jeshi la wanamaji huko Agadez. (Picha ya kielelezo) AP - Carley Petesch
Matangazo ya kibiashara

Inakadiriwa kuwa watu 5,000 ndio waliandamana asubuhi ya Aprili 13 kutoka eneo la Place Toumo lililoko katikati mwa jiji la Niamey. Kulikuwa na wanafunzi hasa wa shule za sekondari na vyuo vikuu. Kambi za jeshi pia zilituma mabasi kuwasafirisha wanajeshi wao katika eneo la Place Toumo kujiunga na waandamanaji.

Wote waliandamana kwa amani, wakifuata viongozi wa maandamano hayo, ambao ni baadhi ya maafisa wa utawala wa kijeshi wa CNSP akiwemo msemaji wake na mkuu wa majeshi binafsi ya Jenerali na Rais Abdourahamane Tiani. Pia walikuwepo wajumbe wa serikali ya mpito ya Niger.

Umati huo uliimba nyimbo za chuki dhidi ya wanajeshi 1,100 wa Kimarekani walio kwenye ardhi ya Niger, wengi wao wakiwa katika kambi ya jeshi la wanaanga ya Agadez. kambi hiyo ni ya kimkakati sana kwa Marekani na idara yake ya ujasusi. Hapa ndipo ndege zake za uchunguzi zisizo na rubani na helikopta hupaa na kutanda eneo lote.

Maandamano yalimalizika kwa mkutano, kwenye eneo kunakopatikana makao makuu ya Bunge.

Mkutano huu unakuja siku tatu baada ya kutua, huko Niamey, wakufunzi wa Urusi ambao waliwasilisha vifaa vya kwanza vya kijeshi, pamoja na mfumo wa ulinzi wa anga, yote ndani ya mfumo wa ushirikiano mpya na Moscow, kulingana na runinga ya umma ya Nigeria.

Maandamano ya Jumamosi hii asubuhi pia yanaunga mkono uamuzi wa serikali ya kijeshi ya CNSP ambayo ilishutumu, mwezi mmoja uliopita, makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.