Pata taarifa kuu

Kenya yapendekeza kuwepo kwa mkataba wa bahari kati ya Ethiopia na Somalia

Kenya imependekeza kuwepo kwa mkataba wa matumizi ya Bahari kati ya Ethiopia na Somalia ili kutatua mvutano kati ya nchi hizo mbili, kufuatia hatua ya serikali ya Addis Ababa kuingia kwenya maelewano na jimbo la Somaliland kuhusu ujenzi wa kambi ya jeshi kwenye ukanda wake wa Pwani, kitendo ambacho kimeikasirisha serikali ya Mogadishu.

Kenya inasema iwapo pendekezo lake litakubalika, litamaliza mzozo huo.
Kenya inasema iwapo pendekezo lake litakubalika, litamaliza mzozo huo. AFP - ED RAM
Matangazo ya kibiashara

Hili limebainishwa na Korir Sing’oei, Katibu kwenye Wizara ya Mambo ya nje, alipozungumza na Shirika la Reuters baada ya rais wa Kenya William Ruto siku ya Alhamisi kukutana na mwenzake wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud kujaribu kutafuta mwafaka wa mvutano huo, baada ya kikao cha viongozi wa IGAD kilichofanyika jijini Kampala mwezi Januari kugonga mwamba, baada ya kususiwa na Ethiopia.

Kenya inasema iwapo pendekezo lake litakubalika, litamaliza mzozo huo na Ethiopia ambayo haina Bahari na itapata ufumbuzi wa kudumu kwa changamoto zake na kuheshimu uhuru wa nchi jirani ya Somalia.

Soma piaWakuu wa IGAD kujadili mvutano kati ya Ethiopia na Somalia

Ripoti zaidi zinasema Somalia na Ethiopia, zinathathmini pendekezo hilo la Kenya na viongozi wa nchi hizo mbili wametarajiwa kukutana na kujadiliana.

Hatua hii inakuja baada ya wiki hii mvutano kati ya nchi hizo mbili kuendelea ambapo Somalia ilimfukuza Balozi wa Ethiopia nchini mwake.

Kenya inaonya kuwa iwapo mzozo huo utaendelea, kundi la kigaidi la Al Shabab, litatumia mwanya huo kuendelea kutekeleza kutekeleza mashambulio dhidi ya uongozi wa Mogadishu kwa madai kuwa imeshindwa kulinda mipaka ya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.