Pata taarifa kuu
MAUAJI-UCHUNGUZI

Afrika Kusini: Watu 6 wakamatwa wiki moja baada ya mauaji ya mwanasoka Luke Fleurs

Polisi ya Afrika Kusini imetangaza siku ya Jumatano kwamba wamewakamata washukiwa sita, wiki moja baada ya mauaji ya mwanasoka Luke Fleurs ambaye aliichezea klabu ya Kaizer Chiefs ya Johannesburg.

Luke Fleurs alikuwa akiendesha gari lake kwenye kituo cha mafuta wakati wanaume wawili walimvamia na kumwamuru atoke nje ya gari hilo wakiwa wakimtishia kwa bunduki.
Luke Fleurs alikuwa akiendesha gari lake kwenye kituo cha mafuta wakati wanaume wawili walimvamia na kumwamuru atoke nje ya gari hilo wakiwa wakimtishia kwa bunduki. © AP
Matangazo ya kibiashara

Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 24 alipigwa risasi wiki iliyopita alipokuwa akijaza gari mafuta lake kwenye kituo cha mafuta katika moja ya vitongoji vya kaskazini-magharibi mwa jiji na kutangazwa kuwa amefariki alipofikishwa hospitalini. "Polisi waliwakamata washukiwa sita kwa jaribio la wizi na mauaji," amesema mwakilishi wa polisi Mavela Masondo.

Kukamatwa kwa watu hao kulifanyika mapema Jumatano katika kitongoji cha Soweto, kusini magharibi mwa Johannesburg, siku mbili baada ya gari la Fleurs kugunduliwa, kulingana na msemaji wa polisui. Chiefs ni moja ya vilabu vikubwa zaidi vya kandanda nchini, mabingwa mara kumi na mbili wa Afrika Kusini, na waliofika fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika mnamo mwaka 2021.

Kulingana na mamlaka, Luke Fleurs alikuwa akingoja kuhudumiwa katika kituo cha mafuta alipokuwa akiendesha gari lake wakati wanaume wawili walipomvamia ndani ya gari lake na kumwamuru atoke nje ya gari hilo wakimtishia kwa bunduki. Mara tu aliposhuka kwenye gari lake, walimpiga risasi kabla ya kukimbia kwenye gari lake.

Wachunguzi wanaamini washukiwa hao ni sehemu ya kundi la uhalifu linalohusika na wizi mwingine wa magari huko Gauteng, mojawapo ya mikoa tisa ya Afrika Kusini. "Msako wa kuwatafuta washukiwa wengine unaendelea," ameongeza msemaji wa polisi.

Afrika Kusini inakabiliwa na kiwango cha uhalifu kinachoongezeka, suala kubwa la kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi wa Mei. Nchi ilirekodi karibu mauaji 84 kwa siku kati ya mwezi Oktoba na Desemba, kulingana na takwimu rasmi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.