Pata taarifa kuu

Wahamiaji 38 wakufa maji baada ya boti yao kuzama karibu na Djibouti

Takriban wahamiaji 38, wakiwemo watoto, walifariki siku ya Jumatatu wakati boti lao lilipozama katika pwani ya Djibouti, kulingana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) siku ya Jumanne. Ubalozi wa Ethiopia nchini Djibouti unabainisha kuwa watu hawa ni Waethiopia. Walikuwa wakielekea Yemen.

Picha hii ya Julai 15, 2019 inaonyesha ufuo ambapo wahamiaji wa Ethiopia wanakusanywa na walanguzi kabla ya kuondoka kwa boti kuelekea Yemen jioni. Obock, Djibouti. Picha ya kielelezo.
Picha hii ya Julai 15, 2019 inaonyesha ufuo ambapo wahamiaji wa Ethiopia wanakusanywa na walanguzi kabla ya kuondoka kwa boti kuelekea Yemen jioni. Obock, Djibouti. Picha ya kielelezo. AP - Nariman El-Mofty
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na ubalozi wa Ethiopia nchini Djibouti, boti hilo "lilipinduka kwenye pwani ya kaskazini mashariki mwa Djibouti siku ya Jumatatu" na ilikuwa ikiwasafirisha "wahamiaji 60 wa Ethiopia kwenda Yemen". IOM inabaini kwamba "miili 38 ilipatikana, ikiwa ni pamoja na watoto", baada ya ajali hii ya boti, pia kumeripotiwa "manusura 22" na watu sita "amao hawajulikani walikpo na wanadhaniwa kuwa wamefariki".

"Njia ya Mashariki", inayochukuliwa na wahamiaji kutoka Pembe ya Afrika kufika Saudi Arabia kupitia Yemen iliyokumbwa na vita, inachukuliwa na IOM kama "mojawapo ya njia hatari zaidi kwa wahamiaji barani Afrika na ulimwenguni." .

Tangu mwaka 2014, takriban watu 1,000 wameuawa au kutoweka kwa kutumia njia hii, kulingana na IOM. Mnamo mwezi wa Novemba 2023, wahamiaji 64 walitoweka, wakidhaniwa wamekufa baharini, wakati wa ajali ya boti kwenye pwani ya Yemen, linakumbusha shirika hili la Umoja wa Mataifa.

Mbali na ajali za boti, wahamiaji wanakabiliwa njiani na hatari za "njaa, hatari za afya", "wasafirishaji na wahalifu wengine", ukosefu wa "huduma ya matibabu, chakula, maji, makazi", linasisitiza shirika hilo.

Waethiopia wanaunda kundi kubwa la wahamiaji wanaofuata njia hii ya mashariki kwa matumaini ya kupata maisha bora nchini Saudi Arabia. Ethiopia, nchi ya pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika, yenye wakaazi milioni 120, imekumbwa na migogoro mingi, imekumbwa na ukame mkubwa katika miaka ya hivi karibuni na uchumi unadhoofika.

"Hata kama ajali ni za mara kwa mara, idadi ya wahamiaji inaendelea kuongezeka," unasikitika ubalozi wa Ethiopia nchini Djibouti, ambao unasisitiza kwamba "safari haramu kwenda Yemen kupitia Djibouti haileti chochote isipokuwa kifo."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.