Pata taarifa kuu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa akamilisha ziara yake ya Afrika nchini Côte d'Ivoire

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Stéphane Séjourné amekamilisha ziara yake ya kwanza barani Afrika nchini Côte d'Ivoire siku ya Jumatatu ambayo ilimpeleka Kenya na Rwanda, fursa ya kukaribisha "ushirikiano wenye usawa" na nchi hii ambayo inasalia kuwa moja ya washirika wakuu wa Paris katika bara hilo.

Kabla ya ziara yake mjini Abidjan, waziri wa Ufaransa alikwenda Nairobi kwa mara ya kwanza Jumamosi ambako pia alizungumza kuhusu nia yake ya "kujenga ushirikiano wenye uwiano", ambao lazima "uwe wa manufaa" kwa nchi za Afrika.
Kabla ya ziara yake mjini Abidjan, waziri wa Ufaransa alikwenda Nairobi kwa mara ya kwanza Jumamosi ambako pia alizungumza kuhusu nia yake ya "kujenga ushirikiano wenye uwiano", ambao lazima "uwe wa manufaa" kwa nchi za Afrika. © Musalia Mudavadi
Matangazo ya kibiashara

"Wanadiaspora wanafanya kazi kubwa sana hapa na Ufaransa, kuunda vizuizi, madaraja kati ya raia wetu kutoka pande mbili. Hii ndio maana ya historia ya uhusiano wetu mpya kati ya nchi hizi mbili: kuwa na ubia ambao ni sawia, kuwa na diaspora ambayo inafanya uhusiano huu kati ya tamaduni zetu na uchumi wetu", ametangaza Bw. Séjourné wakati wa mkutano na waandishi wa habari na Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara.

Akirejelea "matokeo mazuri ya uchumi wa Côte d'Ivoire kwa muongo mmoja", pia ametaja jukumu la Côte d'Ivoire katika "utulivu katika ngazi ya kanda". "Tutaendelea kufanya kazi nanyi kwa utulivu huu," ameongeza. Rais Ouattara, kwa upande wake, alikaribisha "uhusiano wa karibu wa kihistoria wa urafiki na ushirikiano ambao unaendelea kuimarika" kati ya nchi hizo mbili, akiishukuru Ufaransa kwa "uungaji mkono wake katika karibu nyanja zote".

Côte d'Ivoire inasalia kuwa mshirika mzuri wa Ufaransa katika Afrika Magharibi wakati nchi kadhaa katika eneo hilo kama vile Mali, Burkina Faso na Niger, zote zikitawaliwa na tawala za kijeshi zilizoingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi, zimeipa mgongo Paris. Kwa takriban mwaka mmoja, Ufaransa imekuwa ikiangazia nia yake ya kubadilisha uhusiano wake na bara hilo kwa kina, ikisisitiza kuwa inasikiliza maombi ya washirika wa Afrika, haswa kuhusu masuala ya usalama.

Kabla ya ziara yake mjini Abidjan, waziri wa Ufaransa alikwenda Nairobi kwa mara ya kwanza Jumamosi ambako pia alizungumza kuhusu nia yake ya "kujenga ushirikiano wenye uwiano", ambao lazima "uwe wa manufaa" kwa nchi za Afrika. Siku ya Jumapili, alishiriki katika ukumbusho wa miaka 30 ya mauaji ya kimbari ya Watutsi nchini Rwanda. Stéphane Séjourné aalitazamia kuondoka Abidjan Jumatatu jioni kurejea Paris.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.