Pata taarifa kuu

Sudan: Watu 28 wameuawa katika shambulio la RSF

Nairobi – Watu 28 wameuawa baada ya kushambuliwa na wanamgambo wa RSF katika kijiji  cha  Um Adam  umbali wa Kilomita 150 Kusini mwa jiji kuu Khartoum, kwa mujibu wa ripoti za maafisa wa afya.

Mohamed Hamdan Dagalo- Mkuu wa RSF nchini Sudan.
Mohamed Hamdan Dagalo- Mkuu wa RSF nchini Sudan. REUTERS - MOHAMED NURELDIN ABDALLAH
Matangazo ya kibiashara

Mauaji hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki iliopita na kuwaacha watu wengine zaidi ya 240 na majeraha.

Maafisa wa afya wanahofia kuwa huenda idadi ikawa kubwa zaidi kwa sababu hawangeweza kuhesabu idadi kamili ya waliouawa na kujeruhiwa katika shambulio hilo kutokana na ugumu wa kufikia vituo vya afya.

Aidha, chanzo cha matibabu katika hospitali ya Manaqil, kilichopo umbali wa kilomita 80, kiliithibitishia shirika la habari la AFP kwamba wamepokea majeruhi 200, ambao baadhi yao walifika wakiwa wamechelewa.

Kwa mujibu wa  Umoja wa Mataifa, zaidi ya asilimia 70 ya vituo vya afya vya Sudan havina huduma wakati vilivyosalia vinapokea wagonjwa wengi na uwezo wao ni duni.

Vita nchini humo kati ya jeshi, chini ya mkuu wa jeshi Abdel Fattah Al-Burhan, na vikosi vya RSF, chini ya naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Dagalo, vilianza Aprili 15 iliyopita na kufikia sasa maelfu ya watu wameuawa, ikiwa ni pamoja na hadi 15,000 katika mji mmoja eneo lililoharibiwa na vita la Darfur, kulingana na wataalam wa Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.