Pata taarifa kuu

Malawi: Watano waangamia kwa kunywa pombe haramu

Afrika – Watu watano wamefariki jijini Blantyre kusini mwa Malawi huku wengine wawili wakipokea matibabu kwa kunywa pombe iliyo na sumu.

Viwanda vidogo vya kutengeneza bia vimezindua bia zao za kujitengenezea nyumbani.
Viwanda vidogo vya kutengeneza bia vimezindua bia zao za kujitengenezea nyumbani. © Pixabay
Matangazo ya kibiashara

Watu tisa, jinsia ya kiume walikimbizwa katika hospitali kuu ya rufaa ya jiji baada ya kunywa pombe ya kienyeji.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Afya na Huduma za Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Blantyre, Gift Kawalazira, imethibitisha kutokea kwa vifo vya watu watano na kusema wengine wawili wanaendelea na matibabu katika hospitali hiyo.

Malawi imekuwa ikipambana na uuzaji haramu wa pombe ya bei nafuu inayotumiwa zaidi na vijana wasio na ajira na baadhi ya watoto wadogo.

Aina kadhaa za bia za bei nafuu zimepigwa marufuku hapo awali, lakini mamlaka hazijafaulu kuziondoa kabisa sokoni.

Kufuatia vifo hivyo vilivyotokea, polisi wamesema wameanza msako wa watengenezaji pombe na wauzaji wa pombe ya kienyeji inayofahamika kwa majina mbalimbali ya kienyeji yakiwemo "nichukue Bwana", "stagger" na "monkey killer".

Kufikia Jumapili jioni hakuna mtu aliyekamatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.