Pata taarifa kuu

DRC: WFP inalenga kulisha watoto 600,000 wanaokabiliwa na uhaba wa chakula

Shirika la umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP, linasema linahitaji kwa haraka kuwafikia watoto na watu wazima zaidi ya laki 6 nchini DRC wanaokabiliwa na uhaba wa chakula pamoja na utapiamlo.

Picha ya faili ikionyesha wakimbizi wakipiga foleni kupokea chakula cha msaada.
Picha ya faili ikionyesha wakimbizi wakipiga foleni kupokea chakula cha msaada. AFP PHOTO / ROBERTO SCHMIDT
Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo linapanga kutoa chakula cha lishe kwa watoto LAKI 1 na ELFU 48 katika majimbo manne na linakadiria kuwafikia watoto LAKI 6 kufikia mwisho wa mwaka huu.

Watoto ni miongoni mwa watu walio katika hatari zaidi kukosa chakula, ambapo kwa mujibu wa UNICEF karibu asilimi 40 ya raia wa Congo, wanakabiliwa na njaa, utafiti umeonesha.

UNICEF Inakadiria kuwa, idadi ya wakongo wanaohitaji msaada wa chakula itapanda kutoka million 6 na laki 4 hadi million 8 na laki 4 mwaka huu.

Majimbo yaliyoathirika zaidi ni pamoja na Kivu Kaskazini na Ituri, ambayo yanashuhudia kuzorota kwa usalama.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.