Kenya: Ufaransa inalenga kuimarisha uhusiano wake na mataifa ya Afrika
Nairobi – Ufaransa inasema inalenga kuimarisha uhusiano wake na mataifa ya Afrika, utakaoimarisha pande zote kwenye maeneo mbalimbali za ushirikiano wa maendeleo.
Imechapishwa:
Kauli hii imetolewa na Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa, Stephane Sejourne, jijini Nairobi, katika ziara yake ya kwanza barani Afrika kabla ya kuzuru Rwanda na baadaye Cote Dvoire.
Sejourne, amesisitiza nafasi ya Ufaransa kushirikiana na mataifa ya Afrika kama Kenya kutatua changamoto za kikanda hasa mzozo wa Sudan, kuelekea Aprili 15 ambapo Ufaransa itakuwa mwenyeji wa kongamano la Kimataifa kuisaidia Sudan kupata misaada ya kibinadamu.
‘‘Lengo le kwanza ni kuwa mgogoro huo ujadiliwe na kwa hivyo lazima tuhamasishe jumuiya ya kimataifa ili ijue namna ya kufanya maandalizi pamoja na washirika wetu.’’ ameeleza Waziri Stephane Sejourne.
Stephane Sejourne- Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa
Kuhusu mpango wa Kenya kutuma polisi wake nchini Haiti, Sejourne amesema Ufaransa inaunga harakati hizo na imetoa kiasi cha yuro Milioni tatu katika mfuko wa Umoja wa mataifa ili kufadhili operesheni hiyo, ambayo Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya Musalia Mudavadi amesema, Kenya ipo tayari kutoa uongozi.
‘‘Ufaransa kuna mambo mengi wanafahamu kuhusu Haiti na tunataka watusaidie kuelewa zaidi kuhusu oparesheni ya kimataifa ya kurejesha utulivu.’’ alisema Waziri Musalia.
Musalia Mudavadi- Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya
Ziara ya Sejourne nchini Kenya imekuja wakati huu Ufaransa ikiimarisha uwekezaji wake kwenye nchi hiyo yenye uchumi mkubwa Afrika Mashariki, kufuatia ongezeko la kampuni za Ufaransa nchini humo kuongezeka kutoka 50 hadi 140 kwa kipindi cha miaka 10 na kuahidi kuongeza uwekezaji zaidi kwenye mapambano ya mabadiliko ya tabia nchi, miundo mbinu ya uchukuzi na michezo.
We agreed to expedite the implementation of the project cofinanced by both countries to construct 8 sports complexes, using the Agora Model, in various parts of our country, to enhance sports infrastructure and facilitate cohosting of AFCON in 2027. pic.twitter.com/h5kT5faz5d
— Musalia W Mudavadi (@MusaliaMudavadi) April 6, 2024