Pata taarifa kuu

Vikosi vya SADC kuondoka nchini Msumbiji mwezi Julai mwaka huu

Nairobi – Ifikapo Julai 15 mwaka huu, vikosi vya kulinda Amani kutoka jumuiya ya SADC vinatarajiwa kuondoka nchini Msumbiji, ambako vilikuwa vinaisaidia nchi hiyo kukabiliana na wanajihadi wa kiislamu kaskazini mwa nchi hiyo.

Hata hivyo kuanza kuondoka kwao kumeacha hisia mseto kuhusu mafanikio yake kwenye taifa hilo.
Hata hivyo kuanza kuondoka kwao kumeacha hisia mseto kuhusu mafanikio yake kwenye taifa hilo. AFP - ALFREDO ZUNIGA
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo kuanza kuondoka kwao kumeacha hisia mseto kuhusu mafanikio yake kwenye taifa hilo.

Tangu mwaka 2017, vikosi hivyo vilikuwa kwenye jimbo la Cabo Del Gado, kuwadhibiti wanajihadi wa kiislamu wanaojiita Al Sunnah, ambao wameua maelfu ya raia na kusababisha wengine kuyakimbia makazi yao.

Uwepo wao nchini humo, ulitokana na ombi la serikali ya Maputo pamoja na shinikizo la nchi za ukanda zilizoitaka nchi hiyo kuwadhibiti wapiganaji hao kabla ya kuenea katika nchi jirani.

Hata hivyo, wakati huu SADC ikijiandaa kuwaondoa wanajeshi wake, kumekuwa na hofu kuwa huenda wanajihadi hao wakarejea kwa nguvu kutokana na ukweli kuwa, vikosi hivyo havijafanikiwa asilimia 100 kuwamaliza wanajihadi hao.

Kwa wadadisi wa masuala ya usalama, wanaona kuna haja ya wanajeshi hao kuongezewa muda zaidi ili kutoa hakikisho la usalama kwa raia wa kaskazini mwa Msumbiji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.