Pata taarifa kuu

Uganda: Mahakama kutoa uamuzi kuhusu sheria kali dhidi ya ushoga

Nairobi – Mahakama ya katiba nchini Uganda, baadae hivi leo inatarajiwa kutoa uamuzi katika shauri linalotaka ibatilishe sheria kali kuhusu ushoga iliyopitishwa na bunge, sheria ambayo ilisababisha Kampala kukashifiwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Bendera ya LGBTQ
Bendera ya LGBTQ AP - Lee Jin-man
Matangazo ya kibiashara

Wakili wa upande wa walalamishi amefahamisha kuwa uamuzi huo unaweza kusisitiza kuongezeka kwa ukandamizaji dhidi ya mashoga barani Afrika, ikiwa ni pamoja na nchini Ghana ambapo wabunge walipitisha sheria kali dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Mwaka 2022, serikali ya Uganda ilipiga marufuku na kusimamisha shughuli za Shirika linalowatetea mashoga kwa sababu halikuwa imesajiliwa rasmi.

Mahusiano ya watu wa jinsia moja yameharamishwa nchini Uganda tangu enzi ya ukoloni wa Uingereza na nchi hiyo kutunga mojawapo ya sheria kali zaidi duniani dhidi ya LGBT mwezi Mei, na kuharamisha ukuzaji wa ushoga nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.