Pata taarifa kuu

Guinea: Upinzani wataka kurejea kwa raia madarakani kabla ya tarehe 31 Desemba

Vyama vikuu vya upinzani na mashirika ya kiraia nchini Guinea yanaitaka serikali kuanzishwa upya kwa ratiba inayolenga kurejea kwa raia madarakani kabla ya Desemba 31, 2024.

Kiongozi wa upinzani nchini Guinea na Waziri Mkuu wa zamani Cellou Dalein Diallo.
Kiongozi wa upinzani nchini Guinea na Waziri Mkuu wa zamani Cellou Dalein Diallo. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu alitambua katikati ya mwezi wa Machi kwamba ahadi ya jeshi lililoko madarakani tangu 2021, chini ya shinikizo la kimataifa, kutoa nafasi kwa raia kabla ya mwisho wa mwaka 2024 haitaweza kutekelezwa, na kwamba wanapaswa kubaki madarakani angalau hadi mwaka 2025.

Muungano unaoleta pamoja vyama vikuu vya upinzani na mashirika ya kiraia (FVG) "unalaani vikali uamuzi wa utawala wa kijeshi wa Guinea wa kutoandaa, kwa mujibu wa makubaliano yaliyohitimishwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) mwezi wa Oktoba 2022, uchaguzi wa urais mwezi wa Desemba 2024.

"Baada ya zaidi ya miaka miwili ya kipindi cha mpito, Guinea bado haina rasimu ya katiba, wala sheria za uchaguzi, wala bodi ya usimamizi wa uchaguzi, wala daftari (la uchaguzi)," wanashutumu katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Wanashutumu utawala wa kijeshi kwa kuzuia uhuru wa umma na kunyanyasa viongozi wa kisiasa.

Wanatoa wito wa "kurejeshwa kwa uhuru wa umma na kurejea kwa utaratibu wa kikatiba kabla ya Desemba 31", na kuongeza kuwa hawatatambua tena wanajeshi walio madarakani baada ya muda huu wa mwisho.

Kuahirisha mwisho wa kipindi cha mpito bila mashauriano yoyote na wahusika wa kijamii na kisiasa kunahatarisha mazungumzo yoyote na utawala wa kijeshi, wanaongeza.

Muungano huo wa vyama vya siasa na mashirika ya kiraia wanataka kuanzishwa kwa Chombo huru na kilichokubalika cha Usimamizi wa Uchaguzi (OGE), marekebisho na kuwasilishwa kwa kura ya maoni ya Katiba ya zamani ya mwaka 2010, pamoja na marekebisho ya sheria za uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.