Pata taarifa kuu

Ghana: Kasisi mwenye umri wa miaka 63 aoa msichana wa miaka 13

Ndoa ya msichana mwenye umri wa miaka 13 na kasisi mwenye umri wa miaka 63 nchini Ghana imezua sintofahamu katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi na kusababisha wito wa mtu huyo kukamatwa.

Nchini Ghana, umri wa chini kabisa wa ndoa kwa msichana ni miaka 18.
Nchini Ghana, umri wa chini kabisa wa ndoa kwa msichana ni miaka 18. © AFP/Jordi Perdigo
Matangazo ya kibiashara

Kasisi Nuumo Borketey Laweh Tsuru XXXIII, anayejulikana pia kama Gborbu Wulomo, alimuoa msichana huyo katika sherehe ya kitamaduni siku ya Jumamosi karibu na mji mkuu Accra. Polisi na mamlaka awali walisema msichana huyo alikuwa na umri wa miaka 12 au 13, lakini mamlaka husika za kimila zinasema ana umri wa miaka 16.

"Inaonekana tunafikiria mambo machache. Kwa mfano, umri wa miaka 12 ambao tuliaminishwa ni wa uongo. Mtoto anakaribia miaka 16... bado ni mdogo," Waziri wa Masuala ya Kidini Stephen Asamoah Boateng amesema katika mahojiano na kituo cha redio cha ndani.

Picha na video za ndoa hii zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii, na hivyo kuzua hasira miongoni mwa watumiaji wa Intaneti na watetezi wa haki za watoto. Nchini Ghana, umri wa chini kabisa wa ndoa ni miaka 18.

"Serikali lazima ichukue hatua mara moja," Nana Oye Bampoe Addo, mwanaharakati na waziri wa zamani wa Usawa wa Jinsia, Watoto na Ulinzi wa Jamii nchini Ghana, aliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumanne, akisisitiza kuwa mila na desturi haziendani na sheria na Katiba ya Ghana. "Kilichotokea ni uhalifu na ni kinyume cha sheria," aliongeza.

"Ikiwa tuhuma hizo zitathibitishwa, ni kosa la jinai ambalo wote wanaohusika lazima washtakiwe," ofisi ya mwanasheria mkuu, ambayo imefungua uchunguzi, imesema katika taarifa. Mamlaka na polisi wanasema msichana huyo ana umri wa miaka 13, lakini mamlaka za kitamaduni zilizohusika katika sherehe hiyo zinasema ana umri wa miaka 16.

Ili kutetea ndoa hii, msemaji wa kasisi huyo amethibitisha kwamba hakuna suala la mahusiano ya kingono. Bila kutaja umri wa msichana huyo, amesema hakutakuwa na uhusiano wowote wa kimwili hadi afikie umri halali wa kukubalika, uliowekwa kwa miaka 16.

"Sio sherehe ya ndoa. Hakuna uhusiano wowote wa kimwili. Kasisi tayari ana wake watatu wa kimila. Ni jukumu la kimila ambalo ni kumsaidia padre katika majukumu yake ya kiroho," msemaji wake, Mankralo Shwonotalor ameliambia shirika la habari la AFP kwa simu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.