Pata taarifa kuu

Watu kumi wameuawa katika shambulizi jipya linalohusishwa na ADF mashariki mwa DRC

Takriban raia 10 wameuawa katika shambulio jipya linalohusishwa na waasi wa ADF, wenye mafungamano na kundi la Islamic State. shambulio hilo limetekelezwa mchana kweupe katika mji wa mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kulingana na vyanzo vya ndani.

Watu waliotoroka makazi yao wakikimbia eneo la shambulio linalodaiwa kutekelezwa na kundi la waasi la ADF katika kijiji cha Halungupa karibu na Beni, Kivu Kaskazini, DRC, Februari 18, 2020.
Watu waliotoroka makazi yao wakikimbia eneo la shambulio linalodaiwa kutekelezwa na kundi la waasi la ADF katika kijiji cha Halungupa karibu na Beni, Kivu Kaskazini, DRC, Februari 18, 2020. © AFP/Alexis Huguet
Matangazo ya kibiashara

"Leo asubuhi, ADF walifanya uvamizi Mangodomu (katika wilaya ya Mangina katika eneo la Beni), kwa ajili ya kupata dawa na chakula," amesema meya wa Mangina, Emmanuel Kathembo Salamu.

"Walichoma banda la kituo cha afya, walipora maduka na kuchoma nyumba," amesema, na kuongeza kuwa "watu kumi waliuawa katika uvamizi huu."

"Jeshi linamsaka adui (...). Hofu imetanda hapa," meya amebainisha.

ADF ilishambulia kitongoji cha Mangodomu "karibu saa nne asubuhi," amesema Muongozi Kakule Vunyatsi, wa shirika la kiraia "Forces vives de Mangina".

Ripoti ya muda inaonyesha "raia 10 waliuawa ikiwa ni pamoja na mgonjwa katika kituo cha afya", ambapo "pikipiki sita za wauguzi, chumba cha huduma kabla ya kujifungua na veranda zilichomwa moto", ameongeza.

Kapteni Antony Mwalushayi, msemaji wa jeshi katika mkoa huo, hakuthibitisha vifo vya watu 10 lakini amesisitiza kuwa jeshi la DRC (FARDC) "limewaangamiza magaidi wanne" na "kuwakomboa wasichana wanne" ambao walikuwa wametekwa nyara.

"Uingiliaji kati wa jeshi ulichelewa kidogo, askari wetu hapa Mangina hawana hata gari la kukabiliana na adui", amesema Nicaisse Kasereka, rais wa "bunge la vijana" la wilaya.

Kundi la ADF (Allied Democratic Forces), ambalo asili yake ni Waislamu wengi wa waasi wa Uganda, limeanzishwa tangu katikati ya miaka ya 1990 mashariki mwa DRC, ambapo wameua maelfu ya raia.

Walitangaza utii wao kwa kundi la  ISIS mwaka 2019 na pia wanashutumiwa kwa mashambulizi kadhaa ya hivi majuzi katika ardhi ya Uganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.