Pata taarifa kuu

Burundi: Serikali yatakiwa kuacha kuingilia masuala ya chama cha upinzani

Nairobi – Muungano wa viongozi wa upinzani barani Afrika umeelezea hofu yake juu ya kuzorota kwa hali ya haki za binadamu na uhuru wa kiraia nchini Burundi na kuiomba serikali ya Burundi kuacha kuingilia masuala ya ndani ya chama kikuu cha upinzani,CNL.

Agathon Rwasa -Aliyekuwa kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Burundi kabla ya kuondolewa kwenye wadhifa huo.
Agathon Rwasa -Aliyekuwa kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Burundi kabla ya kuondolewa kwenye wadhifa huo. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa vyama vya upinzani kutoka nchini Kenya, Uganda na Tanzania wamekumbusha tamko lao la Machi 9, 2024 ambapo wanaitaka serikali ya Burundi kuheshimu katiba na sheria za nchi pamoja na mikataba ya kikanda na kimataifa ambayo Burundi imetia saini.

Bado kupitia tamko la Machi 9, wanaiomba serikali ya Burundi kuacha kuingilia masuala ya ndani ya chama kikuu cha upinzani, CNL. Tukio hilo linakuja baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Maendeleo ya Jamii na Usalama wa Umma kuridhia kuondolewa kwa Agathon Rwasa kama mkuu wa chama cha National Congress for Liberty (CNL).

Agathon Rwasa aliondolewa katika wadhifa wa kiongozi wa chama kikuu cha upinzani  cha CNL nchini Burundi,.
Agathon Rwasa aliondolewa katika wadhifa wa kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha CNL nchini Burundi,. REUTERS/Thomas Mukoya

Wajumbe katika jukwaa hilo wamebaini maskitiko yao kuona badala ya kuitikia wito wao huo mamlaka ya Burundi tangu wakati huo imezidisha uingiliaji ndani ya chama cha CNL kwa kusaidia kikamilifu kundi la wachache la waasi wa CNL kuchukua udhibiti wa chama kinyume cha sheria.

Kufuatia dhamira ya serikali kutaka kunyakuliwa kinyume cha sheria kwa upinzani rasmi, wanachama hawa wanasisitiza kwa uwazi wanao ushahidi kwamba mnamo Februari 2024, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi alitoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Agathon Rwasa, akimhusisha na vikundi vya kigaidi.

Mbali na kutaka kudhibiti CNL kinyume cha sheria, wanasikitishwa na ukweli kwamba Waziri wa Mambo ya Ndani kwa mara nyingine amemtuhumu, bila ya msingi wowote, kuwa ametuma watu wasiojulikana kupekua nyumbani kwa waziri huyo na kubaini magari 'anayoendesha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.