Pata taarifa kuu

Chad: Wawaniaji 10 wa upinzani wamezuiwa kuwania uchaguzi wa urais

Nairobi – Utawala wa kijeshi nchini Chad, umewazuia wawaniaji 10 wa upinzani kushiriki kwenye uchaguzi wa urais, wa Mei 6, kwa misingi kwamba maombi yao  yalikuwa makosa.

Uchaguzi nchini Chad umepangwa kufanyika Mei sita ili kurejesha utawala wa kiraia.
Uchaguzi nchini Chad umepangwa kufanyika Mei sita ili kurejesha utawala wa kiraia. © AP - Mikhail Metzel
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa waliozuiwa kuwania urais ni pamoja na Nassour Ibrahim Neguy Koursami, Rakhis Ahmat Saleh na Ahmat Hassaballah Soubiane, ambao wamekuwa mstari wa mbele kukosoa utawala wa kijeshi nchini Chad, mahakama ya kikatiba ikisema baadhi ya wagombea waliwasilisha stakabadhi zenye makosa ya majina na sehemu ya kuzaliwa.

Uchaguzi nchini Chad umepangwa kufanyika Mei sita ili kurejesha utawala wa kiraia, baada jeshi kuchukua madaraka mwaka 2021 kufuatia kifo cha rais Idriss Deby.

Wawaniaji wengine 10 akiwemo kiongozi wa kijeshi mwana rais wa zamani Mahamat Idriss Deby Itno, waziri mkuu Succes Masra, aliyekuwa waziri mkuu Albert Pahimi, watachuana kwenye kinyanyiro cha Mei 6.

Tayari upinzani umedai kuwa uchaguzi huo hautakuwa wa huru na haki kutokana na maandalizi yake ambayo umesema yanaegemea utawala wa kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.