Pata taarifa kuu

Rekodi inayozua utata kwa miaka 30 ya Jumuiya ya Kiuchumi na Fedha ya Afrika ya Kati

Jumuiya ya Kiuchumi na Fedha ya Afrika ya Kati (Cemac) inaadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake. Ili kusherehekea hafla hiyo, sherehe inaandaliwa Jumamosi hii, Machi 16, huko Bangui, mji mkuu wa Afrika ya Kati.

Makao makuu ya Cemac huko Libreville, Gabon.
Makao makuu ya Cemac huko Libreville, Gabon. AFP - CELIA LEBUR
Matangazo ya kibiashara

Faustin-Archange Touadéra, rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, lakini pia rais wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Cemac, anatarajia kutoa hotuba yake, hotuba ya kujadili matokeo ya ushirikiano wa kikanda, ripoti inayozua utata miononi mwa nchi wanachama.

Ni miaka thelathini iliyopita, huko N'Djamena, Chad. Nchi sita za Afrika ya Kati (Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kongo-Brazzaville, Equatorial Guinea na Chad) zilianzisha Cemac ili kuongeza biashara na kuoanisha sheria za forodha.

Tangu wakati huo, muda umepita na ni wazi kuwa Cemac inakabiliwa na matatizo mengi. Wengine huzungumza juu ya shirika kama muungano wa kiutawala. Ikiwa hatua zinachukuliwa ili kuhakikisha usafirishaji bure wa bidhaa na watu, kama vile kuanzishwa kwa pasipoti ya nchi wanachama mnamo 2017, kwa kweli mambo ni magumu zaidi.

Ukomo wa mamlaka ya taasisi ndogo za kanda hufanya iwe vigumu kutekeleza maamuzi, jambo ambalo linachochewa na ukosefu wa miundombinu ya barabara na umeme, hasa, ambayo inazuia nchi kuunganishwa vizuri.

Matokeo yake, Cemac ni mojawapo ya kambi ndogo za kiuchumi zilizounganishwa katika bara. Wanachama wake wanafanya biashara 80% na nchi zingine kama China, Urusi na Ulaya, lakini ni 4% tu kati yao. Ushirikiano wa kikanda, ingawa umewekwa katika katiba ya jumuiya hiyo, kwa hivyo bado uko mbali.

Miongoni mwa miradi inayofuata inayosubiri CEMAC, muhimu zaidi bila shaka ni ile ya miradi kumi na tatu shirikishi ambayo ni pamoja na barabara, madaraja na hata miundombinu ya umeme. Ni lazima wafanye iwezekane kuziunganisha nchi wanachama kwa njia bora zaidi.

Novemba mwaka jana, mjini Paris, viongozi wa jumuiya hiyo walitangaza kwamba walikusanya zaidi ya euro bilioni 9 ili kutekeleza miradi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.