Cote Dvoire : Huduma za mtandao wa Internet imeanza kurejea
Nairobi – Huduma za mtandao wa Internet, imeanza kurejea kwenye ukanda wa Afrika ya Kati na Magharibi hasa nchini Cote Dvoire baada ya kushuhudia hitilafu wiki hii, baada ya kukatika kwa nyanya za baharini.
Imechapishwa:
Kampuni ya Internet, MainOne iliyo na ofisi zake nchini Nigeria, Ghana na Cote D’Ivoire, imethibitisha kuanza kurejea kwa huduma hiyo.
Aidha, imethibitisha kuwa hitilafu hiyo ilisababishwa na kukatika kwa nyanya za Internet kwenye Bahari ya Atlantic, Pwani ya eneo la Afrika Magharibi, na kukanusha madai kuwa, ilisababishwa makusudi na watu.
Hata hivyo, ripoti zinasema kuwa huduma hiyo ya Internet inarejea taratibu, lakini kwa kiasi kikubwa hali bado sio nzuri.
Nchini Cote Dvoire ni asilimia 50 ya Internet ndio iliyorejeshwa kwenye kampuni ya mawasiliano ya Orange nchini Cote Dvoire.
Mataifa sita ya Afrika Magharibi, yanayotumia laini ya simu, Djoliba, yaliathiriwa na changamoto hii, kutokana na kuunganishwa kwa mtandao huo kati ya Dakar na Abidjan.