Pata taarifa kuu

Chad: Succès Masra kuwania katika uchaguzi mkuu wa urais

Waziri Mkuu aliyeteuliwa na serikali ya Chad Succès Masra ametangaza kuwa atawania kiti cha urais, tangazo lake likija ikiwa imepita wiki moja tangu kiongozi wa serikali kuu, rais wa mpito Mahamat Déby kutangaza nia yake ya kugombea.

Waziri Mkuu aliyeteuliwa na serikali ya Chad Succès Masra ametangaza kuwa atawania kiti cha urais.
Waziri Mkuu aliyeteuliwa na serikali ya Chad Succès Masra ametangaza kuwa atawania kiti cha urais. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Masra, kiongozi wa zamani wa upinzani, alitia saini mkataba wa maridhiano na rais Déby baada ya kurejea kutoka uhamishoni, kabla ya kuteuliwa kuwa waziri mkuu mwezi Januari.

Kiongozi huyo aliwaambia wafuasi wake katika mkutano wa hadhara siku ya Jumapili kwamba alikuwa ana nia ya kuongoza nchi hiyo ili kuwaunganisha watu.

Upinzani umekosoa hatua hiyo, katika uchaguzi ambao rais Déby anatarajiwa kuibuka mshindi.

Mpinzani mkuu wa Déby, kiongozi wa upinzani Yaya Dillo, aliuawa katika makabiliano ya risasi na vikosi vya usalama tarehe 28 Februari.

Yaya Dillo ndiye aliyekuwa ameonekana kuwa mpinzani mkuu wa  Déby katika uchaguzi huo wa urais.

Déby alichukua wadhifa wa kiongozi wa Chad baada ya babake kuuawa na waasi baada ya kuhudumu kwa miongo mitatu madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.