Pata taarifa kuu

Mali: Roma yatangaza kuachiliwa kwa Waitaliano watatu waliotekwa nyara mnamo 2022

Raia watatu wa Italia kutoka familia moja ambao walitekwa nyara nchini Mali mnamo mwezi Mei 2022 waliachiliwa usiku wa Jumatatu Februari 26 kuamkia Jumanne 27, 2024, serikali ya Italia imetangaza leo Jumanne.

Muonekano wa Palazzo Chigi, huko Roma.
Muonekano wa Palazzo Chigi, huko Roma. AFP - ALBERTO PIZZOLI
Matangazo ya kibiashara

 

"Usiku huu, raia watatu wa Italia wameachiliwa, Rocco Langone, mkewe Maria Donata Caivano na mwanawe Giovanni Langone, waliotekwa nyara Mei 19, 2022," serikali imetangaza katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Raia watatu wa Italia kutoka familia moja ambao walikuwa wametekwa nyara mnamo Mei 19, 2022 karibu na eneo la Koutiala, kusini mwa Mali (sio mbali na mpaka na Burkina Faso), waliachiliwa usiku wa Februari 26 kuamkia 27, 2024, Ofisi ya waziri Mkuu wa Italia imetangaza. "Usiku huu, raia watatu wa Italia waliachiliwa: Rocco Langone, mkewe Maria Donata Caivano na mwanawe Giovanni Langone," Palazzo Chigi amesema katika taarifa kwa vyombo vya habari. "Licha ya kuzuiliwa kwao kwa muda mrefu", wote watatu wako katika "afya njema" na watarejeshwa Roma siku ya Jumanne, amesema.

Familia hiyo, kutoka kundi la kidini la Mashahidi wa Yehova na ambao walikuwa wameishi nchini humo kwa miaka kadhaa, walitekwa nyara na watu wenye silaha kutoka Kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu (Jnim), muungano wa wanajihadi wenye mafungamano na al-Qaeda.

Kuachiliwa kwao kuliwezekana kwa kazi kubwa ya idara ya upelekezi ya Italia kwa "mawasiliano na watu wa kikabila pamoja na idara ya upelelezi ya Mali," serikali imebaini.

Waitaliano hawa watatu walitekwa nyara katika wilaya ya Sincina ka wakati mmoja na raia wa Togo ambaye hakutajwa kwenye taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa mamlaka ya Italia.

Tangu mwaka 2012, Mali inaendelea kukumbwa na kuenea kwa vurugu za wanajihadi na ghasia za kila aina - haswa utekaji nyara wa wageni au Wamali.

(Na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.