Pata taarifa kuu

Wakuu wa ECOWAS kukutana jijini Abuja

Nairobi – Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS, watakutana kesho jijini Abuja, kujadili hali ya kisiasa katika nchi za Niger, Mali na Burkina Faso.

Ajenda kubwa katika kikao hicho, itakuwa ni kuthathmini hatua ya nchi hizo, kutangaza kujiondoa kwenye Jumuiya hiyo mwezi Januari.
Ajenda kubwa katika kikao hicho, itakuwa ni kuthathmini hatua ya nchi hizo, kutangaza kujiondoa kwenye Jumuiya hiyo mwezi Januari. © Nipah Dennis / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ajenda kubwa katika kikao hicho, itakuwa ni kuthathmini hatua ya nchi hizo, kutangaza kujiondoa kwenye Jumuiya hiyo mwezi Januari.

ECOWAS ambayo inapinga hatua hiyo ya nchi hizo kujiondoa kwenye Jumuiya hiyo, inaonya kuwa uamuzi huo utakuwa na madhara ya kiuchumi, kijamii, kiusalama na kisiasa katika ukanda huo.

Aidha, kumekuwa na wasiwasi kuwa uamuzi wa nchi hizo tatu zinazoongowa na wanajeshi, kunahatarisha zaidi hali ya usalama kwenye nchi za Afrika Magharibi na ukanda wa Sahel.

Kuelekea kwenye mkutano huo, aliyewahi kuwa dikteta na kiongozi wa Kijeshi nchini Nigeria, Jenerali Yakubu Gowon, ameonya kuwa uimara wa ECOWAS upo mashakani na ametoa wito kwa viongozi wa Jumuiya hiyo, kuondoa vikwazo dhidi ya Burkina Faso, Guinea, Mali na Niger.

Suala la vikwazo pia linatarajiwa kujadiliwa kwenye kikao hicho jijini Abuja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.