Pata taarifa kuu

Ufaransa yaitaka 'Rwanda kusitisha msaada wowote kwa M23' mashariki mwa DRC

Ufaransa imeitolea wito Rwanda kusitisha msaada wa aina yoyote ile kwa kundi la waasi la M23 linaloendesha harakati zake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Jumatatu Februari 19, 2024, huko Goma, mmoja wa waandamanaji alilaani ukimya wa jumuiya ya kimataifa katika kukabiliana na uingiliaji wa Rwanda kupitia wanamgambo wa M23 mashariki mwa DRC.
Jumatatu Februari 19, 2024, huko Goma, mmoja wa waandamanaji alilaani ukimya wa jumuiya ya kimataifa katika kukabiliana na uingiliaji wa Rwanda kupitia wanamgambo wa M23 mashariki mwa DRC. AFP - GUERCHOM NDEBO
Matangazo ya kibiashara

 

Paris pia inaiomba Kigali, Februari, "kujiondoa kwenye ardhi ya DRC". Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa inapaza sauti yake kuelekea utawala wa Paul Kagame. Hali mashariki mwa DRC ilikuwa kitovu cha mkutano katika Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne jioni.

Paris inatoa wito kwa "Rwanda kusitisha msaada wowote kwa M23 na kujiondoa kwenye ardhi ya Kongo". Quai d'Orsay inasema "inatiwa wasiwasi na hali katika Mashariki mwa DRC, haswa karibu na mji wa Goma na Saké". Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari inaongeza kuwa "mashambulizi dhidi ya utimilifu wa eneo la DRC hayakubaliki" na kwamba "M23 inapaswa kusitisha mapigano mara moja na kuondoka katika maeneo yote inayokalia". Katika taarifa hiyo, Paris imelitaka "jeshi la Kongo kusitisha ushirikiano wote na waasi wa kihutu wa Rwanda wa FDLR".

Kwa tamko hili, Ufaransa inajiweka sawa na msimamo wa Marekani. Jumamosi iliyopita, Marekani ililaani kuongezeka kwa ghasia zinazohusishwa na waasi wa M23. Wizara ya Mambo ya Nje pia ilitoa wito kwa serikali ya Rwanda kuondoa jeshi lake mashariki mwa DRC na kuitaka Kigali "kuondoa mifumo yake ya makombora ya sol air, ambayo ynatishia maisha ya raia, wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wa kibinadamu".

Shutma hizo zinakuja baada ya maandamano ya watu wenye hasira dhidi ya nchi za Magharibi, hasa mjini Kinshasa lakini pia Goma, siku ya Jumatatu Februari 19. Waandamanaji hao walilaani kutojali kwa jumuiya ya kimataifa.

DRC kwenye menyu ya mkutano wa Baraza la Usalama

Kwa upande wao, Jumanne hii jioni, wakati wa mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Marekani ilitoa wito kwa Rwanda na DRC "kuondokana na hatari ya vita". "Jumuiya ya kimataifa lazima ichukue hatua za haraka kukomesha mapigano mashariki mwa DRC na kuwezesha kupunguzwa kwa mvutano kati ya DRC na Rwanda," Naibu Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Robert Wood alisema.

Akizungumza mbele ya Baraza la Usalama, Bintou Keïta, mwakilishi wa Katibu Mkuu nchini DRC, alionya juu ya kuongezeka kwa ghasia na hatari ya kurefushwa kwa mzozo katika eneo hilo, anaripoti mwandishi wetu huko New York, Loubna Anaki.

Akitoa mfano wa hali zinazozunguka Saké na Goma, Bintou Keita alikashifu ukiukaji wa haki za binadamu na sheria za kimataifa unaofanywa na waasi wa M23. Alitaja, kwa mfano, kesi za kuajiri watoto kwa lazima na utekaji nyara wa raia.

Mkuu wa MONUSCO alitoa wito kwa Baraza la Usalama "kutumia nguvu zake zote kusaidia mipango na juhudi za amani".

Kutokana na hali hiyo, wajumbe wa Baraza la Usalama pia walitoa wito kwa pande zote kuheshimu sheria za kimataifa. Ufaransa pia iliitaka Rwanda kusitisha msaada wake kwa M23 na pia ilitangaza kuongezwa kwa wanachama sita wapya wa M23 na FDLR kwenye orodha ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.