Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Mjumbe wa Macron ataja urekebishaji wa uwepo wa jeshi la Ufaransa barani Afrika

Mjumbe binafsi wa rais wa Ufaransa katika bara la Afrika, Jean-Marie Bockel, mezungumza siku ya Jumatano kuhusu "kurekebisha upya" uwepo wa jeshi la Ufaransa nchini Côte d'Ivoire, wakati wa ziara yake mjini Abidjan, ikiwa ni mara yake ya kwanza barani humo tangu aingie madarakani mwanzoni mwa mwezi huu wa Februari.

Waziri wa Utamaduni, Françoise Remarck na Jean-Marie Bockel, baada ya kutembelea Jumba la Makumbusho la Ustaarabu huko Abidjan.
Waziri wa Utamaduni, Françoise Remarck na Jean-Marie Bockel, baada ya kutembelea Jumba la Makumbusho la Ustaarabu huko Abidjan. © Ambassade de France à Abidjan
Matangazo ya kibiashara

"Neno la urekebishaji linaonekana kwangu kama neno sahihi. Dhamira ni kuja na mapendekezo, kusikiliza na kisha mazungumzo ambayo yanaleta makubaliano ya ushindi kwa pande zote mbili", ametangaza Bw. Bockel baada ya mazungumzo ya saa moja " na Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara.

Bw. Bockel, Katibu wa zamani wa Mambo ya Nje wa Ushirikiano chini ya Rais Nicolas Sarkozy (2007-2008), alipewa jukumu mnamo Februari 6 na Emmanuel Macron kujadili na washirika wa Kiafrika aina mpya za uwepo wa jeshi la Ufaransa katika ardhi zao.

Ni nchini Côte d'Ivoire, mmoja wa washirika hodari wa Ufaransa katika Afrika Magharibi, ambayo inawapa hifadhi wanajeshi 900 wa Ufaransa nkatika bataliani ya 43 ya kikosi cha wa Wanamaji (BIMa cha 43), ambako alichagua kufanya ziara yake ya kwanza. "Hatutaki kupunguza juhudi zetu lakini ni jambo la kimataifa: kutakuwa na maendeleo, idadi ya awaajeshi wa ufaransa itakuwa ndogo katika baadhi ya nyanja na itakuwa kubwa kwa nyanja zingine," amesema, bila kutoa maelezo.

"Matarajio ya ushirikiano wetu katika suala la usalama ni matarajio ya kuunga mkono uimarishaji wa kikosi huru cha kijeshi cha Côte d'Ivoire, kupanda kwake kwa kiasi na kwa ubora," ameongeza, akimaanisha "mchakato ambao tayari umeanza.

Wanajeshi wa Ufaransa walifukuzwa kutoka Mali, Burkina Faso na kisha Niger, nchi tatu za Afrika Magharibi zinazotawaliwa na tawala za kijeshi zilizoingia madarakani kupitia mapinduzi na sasa zina uhasama wa wazi kwa Ufaransa. Kwa takriban mwaka mmoja, Paris imekuwa ikiangazia nia yake ya kubadilisha mahusiano yake na bara hilo kwa kina, ikisisitiza kuwa inasikiliza maombi ya washirika wa Afrika, hasa kuhusu masuala ya usalama.

Mbali na Côte d'Ivoire, nchi nyingine tatu za Kiafrika ambazo kunapatikana kambi za wanajshi wa Ufaransa zinahusika na marekebisho haya ya mfumo wa kijeshi: Senegal, Gabon na Chad. Jean-Marie Bockel atawasilisha mapendekezo yake kwa Ikulu ya Elysée mwezi Julai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.