Pata taarifa kuu

Wanajeshi wanane wa Niger na raia mmoja wajeruhiwa katika shambulio karibu na Algeria

Wanajeshi wanane na raia mmoja walijeruhiwa nchini Niger siku ya Jumatano wakati wa shambulio lililofanywa na "majambazi wenye silaha nzito" katika eneo la Agadez (kaskazini), karibu na Algeria, Wizara ya Ulinzi ya Niger imetangaza siku ya Jumamosi.

Mnamo Aprili 2022, wanajeshi wanne waliuawa na watu wenye silaha wasiojulikana huko Djado, eneo linalozalisha dhahabu katika mkoa wa Agadez, kaskazini mwa nchi karibu na Libya.
Mnamo Aprili 2022, wanajeshi wanne waliuawa na watu wenye silaha wasiojulikana huko Djado, eneo linalozalisha dhahabu katika mkoa wa Agadez, kaskazini mwa nchi karibu na Libya. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

 

Shambulio hilo lilifanyika mwendo wa saa 7:00 mchana dhidi ya kikosi cha Wanajeshi wa Niger (FAN) kinachotoa "usindikizaji wa umma" kwenye barabara ya Arlit-Tabarakat, katika eneo la jangwa la Arlit (kaskazini) , kulingana na taarifa ya wizara iliyosomwa kwenye redio ya umma.

Wizara inaripoti wanajeshi wanane na raia mmoja kujeruhiwa wakati wa shambulio hili lililotekelezwa na "majambazi waliokuwa na silaha nzito ndani ya magari tisa ya Toyota". "Jibu" la askari lilifanya iwezekane kusababisha "uharibifu mkubwa wa kibinadamu na vifaa" kwa washambuliaji, kulingana na chanzo hicho, ambacho kinataja kuwa washambuliaji kumi waliuawa na mmoja kukamatwa.

Wizara hiyo inasema jeshi lilipata na kuharibu magari kadhaa ya washambuliaji. Bunduki nne za 12/7, RGP7, bunduki za kivita, kiasi kikubwa cha risasi na nguo za kijeshi pia zilikamatwa, ameongeza.

Eneo la Agadez limejaa migodi ya uchimbaji dhahabu, mengi yao yakiwa ya ufundi, ambayo yanavutia maelfu ya Waniger na raia kutoka nchi jirani. Wizi na mashambulizi mengine dhidi ya wachimba madini ya dhahabu yamekuwa ya mara kwa mara katika eneo la Agadez, ambako vitendo vya ujambazi vimeendelea tangu kumalizika kwa makundi mawili ya waasi ya Tuareg (1991-1995 na 2007-2009).

Mnamo mwezi Juni 2023, washambuliaji watatu waliuawa wakati wa shambulio kwenye vituo vya jeshi karibu na mgodi wa dhahabu huko Tchibarakaten, ambao unapakana na Algeria. Mwaka huo huo, katikati ya mwezi wa Aprili, wanajeshi watano wa Niger waliuawa na watu wenye silaha, walipokuwa wakilinda msafara wa wachimba madini ya dhahabu ambao walikuwa wametoka tu eneo hilo hilo la Tchibarakaten.

Mnamo mwezi Aprili 2022, wanajeshi wanne waliuawa na watu wenye silaha wasiojulikana huko Djado, eneo linalozalisha dhahabu katika mkoa wa Agadez, kaskazini mwa nchi karibu na Libya. Maeneo makubwa ya jangwa, maeneo ya Niger yanayopakana na Libya na Algeria kwa ujumla hayalengwi na wanajihadi, lakini ni njia za usafirishaji wa wahamiaji, silaha na dawa za kulevya, hasa kuelekea Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.