Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-DEMOKRASIA

Senegal: Ufaransa yataka kufanyika kwa uchaguzi 'haraka iwezekanavyo'

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa inatoa wito kwa Senegal leo Jumapili hii, Februari 4, kuondoa "wasiwasi" uliotokana na kuahirishwa kwa muda usiojulikana kwa uchaguzi wa urais, hatua iliyotangazwa siku ya Jumamosi na Rais wa Senegal Macky Sall ili uchaguzi ufanyike "haraka iwezekanavyo."

Rais wa Senegal, Macky Sall, Agosti 17, 2023.
Rais wa Senegal, Macky Sall, Agosti 17, 2023. AFP - EVGENY BIATOV
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa inatoa wito kwa Senegal leo Jumapili hii, Februari 4, kuondoa "wasiwasi" uliotokana na kuahirishwa kwa muda usiojulikana kwa uchaguzi wa urais, hatua iliyotangazwa siku ya Jumamosi na Rais wa Senegal Macky Sall ili uchaguzi ufanyike "haraka iwezekanavyo."

"Tunatoa wito kwa mamlaka kuondoa wasiwasi kuhusu kalenda ya uchaguzi ili uchaguzi ufanyike haraka iwezekanavyo na kwa kufuata sheria za demokrasia ya Senegal," Wizara ya Mambo ya Nje a Ufaransa imesema katika taarifa.

Maandamano yanatarajiwa kufanyika leo Jumapili huko Dakar kwa wito wa upinzani, katika muktadha wa mgogoro mkubwa wa kisiasa.

Wito wa kuandamana

Upinzani nchini Senegal umeitisha maandamano leo Jumapili mjini Dakar na unapanga kuzindua kampeni ya uchaguzi kama ilivyopangwa, na kukataa uamuzi wa Rais Macky Sall.

Tangazo lililotolewa Jumamosi na rais katika muktadha wa mzozo mkubwa wa kisiasa na rais aliyechaguliwa mnamo 2012 na kuchaguliwa tena mnamo 2019 pia lilizua wasiwasi nje ya nchi.

Kwa mara nyingine tena hatua hii inaitumbukiza kusikojulikana nchi hii, inayojulikana kama kisiwa cha utulivu barani Afrika, lakini ambayo imekumbwa na matukio mbalimbali ya machafuko mabaya tangu 2021.

Hatua ya kuahirisha uchaguzi yachukuliwa kwa mara kwanza nchini

Rais Sall alizua mzozo uliozuka kati ya Baraza la Katiba na Bunge la taifa baada ya uthibitisho wa mwisho na mahakama wa wagombea 20 na kuondolewa kwa dazeni kadhaa ili kuhalalisha uamuzi wake. Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka wa 1963 kwa uchaguzi wa urais kupitia kura ya moja kwa moja ya wote kuahirishwa nchini Senegal.

Kulingana na kanuni za uchaguzi, agizo linaloweka tarehe ya uchaguzi mpya wa urais lazima lichapishwe kabla ya siku 80 kabla ya uchaguzi, hali ambayo itasababisha mwisho wa mwezi Aprili katika hali bora zaidi, kwa tukio lisilo wezekana.

Kwa hivyo kuna hatari Rais Sall kusalia kwenye wadhifa wake, baada ya muhula wake kumalizika mnamo Aprili 2.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.