Pata taarifa kuu

Uchaguzi nchini Senegal waahirishwa kwa muda usiojulikana

Rais wa Senegal Macky Sall, anayemaliza muda wake, ametangaza kuwa uchaguzi mkuu uliokuwa umepangwa kufanyika tarehe 25 mwezi huu, umeahirishwa kwa muda usiojulikana.

Rais  Macky Sall  akilihotubia taifa Februari 3 2024.
Rais Macky Sall akilihotubia taifa Februari 3 2024. © Capture d'écran Facebook / Macky Sall
Matangazo ya kibiashara

Akilihotubia taifa siku ya Jumamosi, rais Sall amesema ametia saini hati ya kuahirishwa  kwa uchaguzi huo na kuagiza wabunge kuwachunguza Majaji mawili Baraza la Katiba baada ya sifa zao za utendaji kutiliwa shaka kufuatia zoezi la kuwapata wagombea wa urais.

Hatua hii imekuja baada ya chama Senegalese Democratic Party (PDS)  chake rais wa zamani Abdoulaye Wade, siku ya Ijumaa kuwasilisha mswada bungeni kutaka uchaguzi huo uahirishwe kwa madai kuwa, mazingira yaliyopo yanatilia shaka, uchaguzi huo kuwa huru na haki.

Mgombea wa chama hiki Karim Wade, alizuiwa kuwa miongoni mwa wagombea 20 waliopitishwa na Baraza la Katiba baada ya kubainika kuwa alikuwa hajafuta uraia wake wa Ufaransa.

Hata hivyo, baadhi ya wanasiasa wakiongozwa na mmoja wa wagombea Khalifa Sall, amekuwa akipinga mapendekezo ya uchaguzi huo kuahirishwa kwa madai kuwa iwapo utaahirishwa, utavuruga hali ya kisiasa nchini humo.

Kampeni nchini Senegal zilikuwa zimepangwa kuanza siku ya Jumapili.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.