Pata taarifa kuu

Kongamano la Afrika- Italia linafanyika jijini Rome

Nairobi – Baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika wanakutana jijini Rome Italia, kuhudhuria kongamano la Afrika- Italia ambalo linalenga kuimarisha uhusiano kati ya Afrika na taifa hilo la bara Europa.

Kongamano la nchi za Afrika na Italia linafanyika jijini Rome
Kongamano la nchi za Afrika na Italia linafanyika jijini Rome REUTERS - REMO CASILLI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu waziri mkuu wa Italia, Giorgia Meloni , nchi yake inalenga kutumia mkutano huo wa kilele wa siku mbili kuzindua mbinu mpya ya kushirikiana na nchi za Afrika kwa manufaa ya pande zote.

Mojawapo ya sekta zinazotarajiwa kujadiliwa katika mkutano huo ilikupata  ushirikiano zaidi  ni pamoja na nishati, maendeleo ya kiuchumi na miundombinu, utamaduni, usalama wa chakula, elimu na mafunzo yenye viwango vya juu.

Mkutano huo ulioanza Jumapili, unalenga pia kukuza uwekezaji katika nchi za Afrika kama mkakati wa kuzuia uhamiaji usio wa kawaida kutoka bara hilo kwenda barani Ulaya.

Mataifa mengine kadhaa yameandaa mikutano ya aina hiyo ili kuimarisha uhusiano na nchi za Afrika, zikiwemo Ujerumani, Urusi na China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.