Pata taarifa kuu

Rais wa Chad mjini Moscow kukutana na Putin

Mkuu wa utawala wa kijeshi na rais wa mpito nchini Chad, Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno, aliondoka N'Djamena siku ya Jumanne kwa ziara rasmi nchini Urusi "kwa mwaliko" wa mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, nchi hizo mbili zimetangaza.

Mahamat Déby alitangazwa kuwa mkuu wa nchi na jeshi, akiwa mkuu wa utawala wa kijeshi wa majenerali 15, Aprili 20, 2021 kufuatia kifo cha baba yake, Idriss Déby Itno, aliyeuawa na waasi akiwa njiani kuelekea uwanja wa vita baada ya kutawala Chad kwa mkono wa chuma kwa miaka 30.
Mahamat Déby alitangazwa kuwa mkuu wa nchi na jeshi, akiwa mkuu wa utawala wa kijeshi wa majenerali 15, Aprili 20, 2021 kufuatia kifo cha baba yake, Idriss Déby Itno, aliyeuawa na waasi akiwa njiani kuelekea uwanja wa vita baada ya kutawala Chad kwa mkono wa chuma kwa miaka 30. © AFP - DENIS SASSOU GUEIPEUR
Matangazo ya kibiashara

 

Jenerali Déby "aliondoka N'Djamena asubuhi ya leo kuelekea Moscow. Kwa mwaliko wa Rais (...) Vladimir Putin. Mkuu wa nchi anafanya ziara rasmi katika mji mkuu wa Urusi", ofisi ya rais wa Chad iliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook siku ya Jumanne.

Kremlin imethibitisha ziara hiyo iliyotangazwa katika dakika za mwisho kabisa na N'Djamena, na mkutano uliopangwa kufanyika Jumatano kati ya wawili hao, ambao watazungumza juu ya "matarajio ya maendeleo ya uhusiano wa Urusi na Chad katika nyanja tofauti, na kikanda na kimataifa ya sasa", kulingana na taarifa kutoka kwa ofisi ya rais wa Urusi.

Chad, ambako bao kuna wanajeshi wa Ufaransa, ni mshirika wa mwisho wa Ufaransa katika Sahel, baada ya kulazimishwa na kuondoka kwa lazima kwa wanajeshi wa Ufaransa nchini Mali mnamo mwezi wa Agosti 2022, nchini Burkina Faso mnamo mwezi wa Februari 2023 na nchini Niger mnamo mwezi wa Desemba mwaka uliyopita. Kila moja ya nchi hizi tatu zimeamua kuimarisha uhusiano na Urusi kwa wakati mmoja, hasa katika sekta ya kijeshi.

Tangu mwaka 2013 na hadi wakati huo, hasa na Operesheni yake ya Barkhane iliyomalizika mnamo 2022, Ufaransa ilikuwa nguzo ya muungano wa kijeshi unaojumuisha nchi hizi tatu na Chad, katika vita dhidi ya wanajihadi, hasa katika eneo la mipaka mitatu inayojumuisha Mali, Niger na Burkina Faso. Urusi, hasa kupitia mamluki kutoka kampuni ya kibinafsi ya Wagner, pia iko na ushawishi mkubwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Libya na Sudan, nchi tatu zinazopakana na Chad.

Mahamat Déby alitangazwa kuwa mkuu wa nchi na jeshi, akiwa mkuu wa utawala wa kijeshi wa majenerali 15, Aprili 20, 2021 kufuatia kifo cha baba yake, Idriss Déby Itno, aliyeuawa na waasi akiwa njiani kuelekea uwanja wa vita baada ya kutawala Chad kwa mkono wa chuma kwa miaka 30.

Jenerali huyo kijana mwenye umri wa miaka 37 wakati huo, ambaye jeshi lake linachukuliwa kuwa nguzo ya vita dhidi ya wanajihadi katika eneo hilo, mara moja alishinikizwa na jumuiya ya kimataifa, hususan Paris, baada ya kuahidi kurejesha mamlaka kwa raia. mwisho wa kipindi cha "mpito". Miezi 18 baadaye, alisogeza mbele arehe hii kwa miaka miwili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.