Pata taarifa kuu

DRC: FARDC kushirikiana na wanajeshi wa SADC katika vita dhidi ya M23

Nairobi – Jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limetangaza kuanzisha operesheni ya pamoja na wanajeshi wa kikosi cha Jumuiya ya nchi za SADC dhidi ya waasi wa M23 Mashariki mwa nchi hiyo na kwamba linategemea kikosi hicho kwa kuwatimua waaasi hao wa M23.

Wanajeshi wa DRC kushirikiana na wale wa SADC katika vita dhidi ya waasi wa M23
Wanajeshi wa DRC kushirikiana na wale wa SADC katika vita dhidi ya waasi wa M23 © SADC
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza wakati wa mkutano na wanahabari katika mji mkuu wa mkoa wa Kivu kaskazini, Goma, kaimu mkuu wa jeshi la Congo Luteni Jenerali Fall Sikabwe amesema raia wafahamu kwamba SADC imekuja kwa mapambano, na kwamba jeshi la FARDC na kikosi cha SADC maafuru SAMIDRC wataanzisha operesheni ya pamoja dhidi ya waasi wa M23 tofauti na Kikosi cha EAC.

 

Sikabwe aliongeza kusema kuwa DRC inawategemea wanajeshi kutoka kanda ya kusini mwa Afrika kusaidia kurejesha nguvu na kuhakikisha wanamgambo wa M23 ambao wamedhibiti maeneo kadhaa baada ya mapigano makali dhidi ya jeshi la FARDC likishirikiana na wapiganaji wazalendo mashariki mwa nchi hiyo.

 

Wanajeshi kutoka nchi 10 za Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika (SADC) wamekuwa wakiwasili DRC tangu katikati ya mwezi Desemba, wengi wao kutoka Afrika Kusini, Tanzania na Malawi.

 

Kutumwa kwa jeshi la kikanda kuliamuliwa katika mkutano wa kilele wa SADC mwezi Mei mwaka jana, baada ya Kinshasa kuhoji kuhusu utendakazi wa kikosi cha EAC kilichoonekana kushirikiana na waasi wa M23 badala ya kupigana nao, hali ambayo ilisababisha kutoongezwa kwa muda wa kikosi mashariki mwa nchi hiyo.

 

DRC pia imeomba kuondolewa kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa ambacho kimeanza, waziri wa mambo ya nje alisema Jumamosi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.