Pata taarifa kuu

Morocco kuongoza kitengo cha haki za binadamu UN

Nairobi – Balozi wa Morocco jijini Geneva, amechaguliwa kuwa rais mpya wa Tume ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka wa 2024.

Huu ni mwaka wa Afrika, kuwa rais wa Tume hiyo
Huu ni mwaka wa Afrika, kuwa rais wa Tume hiyo © VALENTIN FLAURAUD / AFP
Matangazo ya kibiashara

Omar Zniber amepata kura 30 na kumshinda mpinzani wake, Mxolisi Nkosi, kutoka nchini Afrika Kusini, aliyepata kura 17.

Huu ni mwaka wa Afrika, kuwa rais wa Tume hiyo, lakini kabla ya zoezi la kupiga kura, mataifa ya Afrika yalishindwa kuelewana ni mgombea yupi aungwe mkono.

Baada ya ushindi huo, Balozi huyo kutoka Morocco, ameahidi kutetea mkataba huo unaotetea haki za binadamu kwa ajili ya mataifa yote.

Wizara ya Mambo ya nje ya Morocco imesema, mgombea wake ameibuka mshindi licha ya Afrika Kusini na Algeria, kuwa kikwazo.

Morocco inasema ushindi wa Balozi wake ni ujumbe mzito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuhusu namna inavyoshughulikia tofauti za kidini, ubaguzi wa rangi na inavyoshughulikia wahamiaji.

Wakosoaji wa nchi hiyo ya Kaskazini mwa barra la Afrika , wamekuwa wakiikosoa Morocco kwa kuwahangaisha wanahabari na wanaharakati wa kutetea haki wa binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.