Pata taarifa kuu

Gambia:Kesi dhidi ya Ousman Sonko kuendelea nchini Uswisi

Nairobi – Mahakama nchini Uswisi katika uamuzi wake imeruhusu kuendelea kwa kesi dhidi ya waziri wa zamani nchini Gambia Ousman Sonko, anayehusishwa na madai ya mauaji, kuwatesa watu pamoja na kuwabaka wanawake.

Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa kwa kipindi cha mwezi mmoja kabla ya uamuzi kufanyika mwezi Machi
Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa kwa kipindi cha mwezi mmoja kabla ya uamuzi kufanyika mwezi Machi © REUTERS / GAMBIA STATE HOUSE WEBSITE / GRTS
Matangazo ya kibiashara

Sonko kwa upande wake amekana madai hayo yanayodaiwa kutekelezwa wakati wa utawala wa rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh.

Mahakama hiyo hapo jana Jumanne, ilitupilia mbali ombi la mawakili wa upande wa utetezi kuwa haikuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Sonko alienda uhamishoni nchini Uswisi mwaka wa 2016 ambapo ameshtakiwa chini ya sheria inayoruhusu mtu kushtakiwa hata kama madai anayokabiliwa nayo yalifanyika kwengine.

Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa kwa kipindi cha mwezi mmoja kabla ya uamuzi kufanyika mwezi Machi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.