Pata taarifa kuu

SADC yaanza kutuma vikosi vyake Mashariki mwa DRC

Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC, imetuma vikosi vyake Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya kuondoka kwa kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Eneo la Masisi, Mashariki mwa DRC mojawapo ya ngome ya waasi wa M 23
Eneo la Masisi, Mashariki mwa DRC mojawapo ya ngome ya waasi wa M 23 © ALEXIS HUGUET / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya SADC kutangaza hatua hiyo mwezi Mei, wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi uliofanyika nchini Namibia.

Siku ya Jumatano, kikosi hicho kikiongozwa na wanajeshi kutoka Afrika Kusini,  kinaripotiwa kuwasili mjini Goma, wakati huu maswali mengi yakisalia kuhusu kuja kwa kikosi hicho.

Hata hivyo, haijafamika rasmi  idadi kamili ya wanajeshi waliowasili lakini ripoti zinasema, hawazidi mia mbili.

Wanjeshi wengine kutoka Tanzania na Malawi, wanatarajiwa kuwasili lakini mpaka sasa haijafahamika lini na idadi yao.

Taarifa ya ndani, kutoka SADC ambayo RFI imeona, iliyoandikwa Desemba 14 inaeleza kuwa, kikosi hicho kitakuwa na operesheni ya miezi 12 na kitakuwa na wanajeshi Elfu Saba.

Kikosi cha SADC kinatarajiwa kupambana na makundi yenye silaha Mashariki mwa nchi hiyo, na kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya nje, lengo lao kubwa itakuwa ni kupigana na M23 jimboni Kivu Kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.