Pata taarifa kuu

Baada ya Uganda, kiongozi wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo azuru Ethiopia

Kiongozi wa kundi ya wapiganaji wa RSF, Mohamed Hamdan Dagalo amewasili hivi leo nchini Ethiopia, katika ziara ya nadra nje ya nchi tangu mapigano kuzuka nchini Sudan mwezi Aprili mwaka huu.

Kiongozi wa kundi ya wapiganaji wa RSF, Mohamed Hamdan Dagalo
Kiongozi wa kundi ya wapiganaji wa RSF, Mohamed Hamdan Dagalo REUTERS - MOHAMED NURELDIN ABDALLAH
Matangazo ya kibiashara

Dagalo maarufu pia kama Hemedti, anazuru Ethiopia baada yake kufanya ziara nchini Uganda siku ya Jumatano na kukutana na rais Yoweri Museveni, na inakuja wakati ambapo wanadiplomasia wa kikanda waking’ang’ania kuwa wapatanishi katika ya jeshi ya Sudan na RSF.

Hemedti baada ya kwa na mazunguymzo na rais Museveni, alisema aliweka hadharani maono yao ya kushiriki kwenye majadiliano, kusitisha vita na kujenga upya taifa la sudan kwa misingi ya haki.

Majerali hasimu, Abdel Fattah al Burhan na Mohamed Dagalo walitakiwa kukutana hivi leo ana kwa ana, nchini Djibouti, lakini hilo halijafanyika, jeshi la Sudan likiilaumu RSF kwa kuchelewesha upatikanaji wa amani.

Tangu kuzuka kwa makabiliano kati ya vikosi vyao, mwezi Aprili, zaidi ya watu elfu 12 wameuawa, huku mamilioni wakikimbia nyumba zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.