Pata taarifa kuu

Takriban watu 15 wafariki katika mlipuko wa lori la mafuta Liberia

Takriban watu 15 walifariki siku ya Jumanne katika mlipuko wa lori la mafuta katikati mwa Liberia, polisi wameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatano.

Ajali kama hizi hutokea mara nyingi katika nchi nyingi barani Afrika. hapa ilikuwa mwaka wa 2010, mlipuko wa lori la mafuta ulisababisha vifo vya zaidi ya watu 230 na karibu mia kujeruhiwa nchini DRC.
Ajali kama hizi hutokea mara nyingi katika nchi nyingi barani Afrika. hapa ilikuwa mwaka wa 2010, mlipuko wa lori la mafuta ulisababisha vifo vya zaidi ya watu 230 na karibu mia kujeruhiwa nchini DRC. RFI / Sébastien Nemeth
Matangazo ya kibiashara

"Watu wengi waliteketea kwa moto. Kwa sasa, tunashikilia idadi ya waliofariki kuwa 15," ameongeza Prince B. Mulbah, naibu inspekta jenerali wa polisi. Lori hiyo ya mafuta ilipinduka na kuanguka kwenye mtaro kando ya barabara huko Totota, Kaunti ya Bong.

"Lori la mafuta lililokuwa likisheheni petroli lilipinduka na watu katika eneo hilo wakaanza kuchota mafuta, hali iliyopelekea lori hilo kulipuka na kuua na kujeruhi watu wengi," Malvin Sackor, afisa mwingine wa polisi ameliamia shirika la habari la AFP. Zaidi ya watu 30 walijeruhiwa, amesema, akibainisha kwamba polisi ilikuwa bado inahesabu idadi ya waathiriwa.

"Watu walipanda lori kupata mafuta ya petroli. Baadhi yao walikuwa na vyuma na walikuwa wakiigonga lori la mafuta ili liweze kupasuka na waweze kupata petroli," ameliambia shirika la habari la AFP Aaron Massaquoi, ambaye anasema alikuwa shahidi wa tukio hilo. Kulingana na Bw. Massaquoi, lori hilo la mafuta liliposhika moto, watu waliokuwa juu waliungua kiasi cha kutotambulika.

Afisa wa Afya wa Kaunti ya Bong Dk. Cynthia Blapooh ameliambia Gazeti la nchini humo la Front Page Africa: "Bado tuna wagonjwa wengi walioathirika sana, wakiwemo watoto na mwanamke mjamzito, jumla ya watu 36."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.