Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Misri yajiandaa kwa uchaguzi wa urais katikati ya mzozo wa kiuchumi

Misri inajiandaa kwa uchaguzi wa urais ambao utamfanya Rais anayemaliza muda wake Abdel Fattah al-Sissi kushinda muhula wa tatu, licha ya kuongezeka minung'uniko ya raia kutokana na hali mbaya ya kiuchumi.

Katika uchaguzi wa 2014 na 2018, Abdel Fattah al-Sissi alipata 96% ya kura.
Katika uchaguzi wa 2014 na 2018, Abdel Fattah al-Sissi alipata 96% ya kura. © AP/Christophe Ena
Matangazo ya kibiashara

Kuanzia Jumapili hadi Jumanne, Wamisri walio na umri wa zaidi ya miaka 18 watalazimika kuchagua kati ya wagombea wanne: Abdel Fattah al-Sissi madarakani tangu alipompindua mwanaharakati wa Kiislamu Mohamed Morsi mwaka 2013, na wagombea wengine watatu ambao kwa ujumla sio maarufu.

Katika nchi hii yenye watu wengi zaidi katika ulimwengu wa Kiarabu, yenye wakazi karibu milioni 106, mfumo unaonekana kuwa wa kifarano: baadhi ya vituo 9,400 vya kupigia kura, wafanyakazi 15,000 wa mahakama walihamasishwa na muda wa kupiga kura wa siku tatu. Matokeo yatatangazwa Desemba 18, isipokuwa duru ya pili ni muhimu. Hali hii hata hivyo inaonekana kutowezekana kwa kuzingatia chaguzi za mwaka 2014 na 2018 ambapo Bw. Sisisi alipata 96% ya kura.

Kwa uchaguzi huu mpya, waangalizi wengine wanaamini kwa muda kuwepo kwa ushindani mkali. Lakini viongozi hao wawili wa upinzani ambao walinuia kubadili hali hiyo, bila ya kuwa na matumaini ya kweli ya kushinda bali kutoa sauti pinzani angalau kwa muda wote wa kampeni, wako gerezani au wanasubiri kesi.

Zaidi ya suala la haki za binadamu - Misri ni ya 135 kati ya nchi 140 katika orodha ya sheria ya World Justice Project - kipaumbele nambari moja kwa Wamisri ni hali ya kiuchumi.

Mfumuko wa bei umefikia 40%, kushuka kwa thamani kwa 50% kumesababisha bei kupanda na sekta binafsi inaendelea kudorora. Ruzuku ya umma inatoweka moja baada ya nyingine chini ya shinikizo kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

"Kuachiliwa kwa wafungwa wa maoni"

IMF bado inasubiri kuweza kufanya tathmini zake za robo mwaka baada ya mkopo mpya kwa Misri, nchi ya pili duniani iliyo katika hatari ya kushindwa kulipa, kulingana na Bloomberg.

Akifahamu matarajio ya kiuchumi ya wapiga kura, mgombea Hazem Omar alibainisha kwamba "uamuzi wake wa kwanza" akichaguliwa utakuwa "udhibiti wa mfumuko wa bei kwa kuondoa VAT kwenye vyakula vya msingi". Alikuwa akizungumza wakati wa mdahalo pekee wa televisheni kati ya wagombea, ambapo Bw. Sissi alimtuma mwanachama wa kampeni yake kumwakilisha.

Mgombea mwingine, Farid Zahran, mkuu wa chama kidogo cha mrengo wa kushoto, aliahidi "kuachiliwa kwa wafungwa wote wa maoni", wanaokadiriwa kuwa maelfu tangu Bw. Sissi aingie madarakani, na "kuondolewa kwa sheria kandamizi".

Kwa Mpango wa Mageuzi ya Waarabu, "Bwana Sissi labda anatumai kwamba vita vya Gaza vitamletea shinikizo kwenye Ghuba na Magharibi", kwa sababu yeye ni mpatanishi muhimu katika mzozo wa Israeli na Palestina, huku akitafuta kuungwa mkono na "wafadhili wa kimataifa ili kupunguza mzozo wa kiuchumi."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.