Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Achraf Hakimi akabiliana na mwanamke anayemtuhumu kwa ubakaji

Mlinzi wa kimataifa wa Morocco anayeichzea klabu ya Paris SG, Achraf Hakimi, amekabiliwa siku ya Ijumaa na mwanamke anayemtuhumu kwa ubakaji, ofisi ya mwendesha mashtaka wa Nanterre imeliambia shirika la habari la AFP.

Mmorocco Achraf Hakimi amekuwa akiichezea PSG tangu 2021.
Mmorocco Achraf Hakimi amekuwa akiichezea PSG tangu 2021. PSG via Getty Images - Aurelien Meunier - PSG
Matangazo ya kibiashara

"Leo asubuhi kulikuwa na makabiliano kati ya mshtakiwa na mlalamikaji" mwenye umri wa miaka 24 ambaye alimshtaki Machi mwaka jana kwa kumbaka siku chache zilizopita, amesema mwendesha mashtaka wa umma. Mchezaji huyo hakuwepo kwenye mazoezi ya PSG siku ya Ijumaa asubuhi kwa "sababu za kibinafsi", kulingana na taarifa ya klabu kwa vyombo vya habari. Mpambano huu unakuja siku chache tu kabla ya mechi ya mchujo katika Ligi ya Mabingwa kwa klabu hiyo ya Paris, ambayo lazima ishinde Dortmund Jumatano ili kujihakikishia nafasi yake katika hatua ya 16 bora.

Mnamo Machi 3, 2023, Achraf Hakimi alishtakiwa kwa ubakaji na jaji wa uchunguzi na kuwekwa chini ya uangalizi wa mahakama. Siku chache mapema, mwanamke mmoja alimshtaki kwa kumbaka siku ya Jumamosi ya wiki iliyopita nyumbani kwake Boulogne-Billancourt (Hauts-de-Seine). "Mteja wangu anashikilia taarifa zake zote na amekuwa mshiriki katika kesi hii," mwanasheria wa mlalamikaji, wakili Rachel-Fleur Pardo ameliamia shirika la habari la AFP.

Mnamo mwezi Machi, kulingana na chanzo cha polisi, mwanamke huyo alisema alikutana na Achraf Hakimi mnamo mwezi Januari kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram na akaenda nyumbani kwake Jumamosi kwa VTC iliyoagizwa na mchezaji. Anadai kuwa Achraf Hakimi alimbusu na kumgusa bila ridhaa yake, kabla ya kumbaka, kiliongeza chanzo cha polisi. Baada ya kufanikiwa kumsukuma, anasema kwamba rafiki, aliyewasiliana naye kupitia ujumbe mfupi wa SMS, alikuja kumchukua.

Wakili wa mchezaji huyo Fanny Colin kisha akahakikisha kwamba tuhuma hizo ni za "uongo". Mashtaka yake yalimpa "hatimaye fursa ya kujitetea", wakili wake alitoa hoja katika taarifa kwa vyombo vya habari, na hasa "kusoma faili". Mchezaji huyo "anakanusha kwa uthabiti" shutuma hizo na "aliyehusika na jaribio la ulaghai" katika jambo hili, amesema.

Achraf Hakimi,kiungo wa timu ya Morocco, anachukuliwa kuwa mmoja wa mabeki bora wa winga ya kulia duniani na aliteuliwa mapema Desemba kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.