Pata taarifa kuu

Mvua kubwa inazidi kunyesha Afrika Mashariki kutokana na shughuli za binadamu

Mvua kubwa ambazo zimeathiri Afrika Mashariki tangu mwezi Oktoba, na kuua zaidi ya watu 300, zimeongezeka maradufu kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na shughuli za binadamu, kulingana na utafiti wa kisayansi uliochapishwa siku ya Alhamisi.

Kaunti ya Mombasa ni mojawapo ya maeneo yalioathirika zaidi ya mafuriko hayo
Kaunti ya Mombasa ni mojawapo ya maeneo yalioathirika zaidi ya mafuriko hayo REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Hali mbaya ya hewa iliyokumba Ethiopia, Kenya na Somalia kati ya mwezi Oktoba na Desemba "ilikuwa kali zaidi katika rekodi katika eneo hilo," kulingana na World Weather Attribution (WWA), mtandao wa kimataifa wa wanasayansi ambao unachambua matukio mabaya ya hali ya hewa kwa wakati halisi.

Kwa mujibu wa watafiti wa WWA, "mabadiliko ya hali ya hewa yalichangia tukio hilo, na kufanya mvua kubwa hadi mara mbili zaidi", na kuongeza "kwamba mradi tu sayari inaendelea kuwa na joto, mvua kubwa kama hizi zitakuwa nyingi zaidi katika Afrika Mashariki.

Ripoti ya WWA imeonyesha "haja ya dharura ya kuondoa nishati ya mafuta na kupunguza uzalishaji hadi sifuri." Watafiti wanabainisha, hata hivyo, kwamba bado kuna "kutokuwa na uhakika" kuhusu "mchango kamili" wa ongezeko la joto duniani.

Pembe ya Afrika ni moja wapo ya maeneo yaliyo hatarini zaidi na mabadiliko ya tabianchi na hali mbaya ya hewa inazidi kuwa ya mara kwa mara na kali. Ukame mbaya zaidi katika miongo minne umekumba eneo hilo baada ya misimu kadhaa ya mvua iliyokatisha tamaa ambayo ilisababisha mamilioni ya watu kua na mahitaji mengi na kuharibu mazao na mifugo.

Kulingana na utafiti wa WWA, watu kuwa katika shida pia kuna "jukumu kubwa": "Jumuiya nyingi zilikuwa tayari zinakabiliwa na ukame wa miaka mitatu uliosababishwa na mabadiliko ya tabianchi, baada ya kusababisha vifo vya mifugo, mavuno duni na uhaba wa chakula.

Mvua kubwa imesababisha zaidi ya watu milioni mbili kuyahama makazi yao katika Afrika Mashariki, karibu nusu yao nchini Somalia pekee. Mvua hiyo ilisababisha vifo vya takriban watu 57 nchini Ethiopia, zaidi ya mia moja wamefariki Somalia na takriban 165 nchini Kenya. Takriban watu 23 pia wamefariki kutokana na ugonjwa wa kipindupindu katika eneo la mashariki mwa Ethiopia lililokumbwa na mafuriko makubwa.

El Niño, ambayo kwa kawaida inahusishwa na ongezeko la joto, ukame katika baadhi ya maeneo ya dunia na mvua kubwa katika maeneo mengine, inatarajiwa kudumu hadi mwezi Aprili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.