Pata taarifa kuu

DRC: Kada wa chama cha Moïse Katumbi afariki baada ya msafara wao kushambuliwa Kindu

Kada wa chama cha mwanasiasa wa upinzani Moïse Katumbi aliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa siku ya Jumanne Novemba 28, 2023 huko Kindu, mashariki mwa DRC, ambapo mwanasiasa huyoi alifika kama sehemu ya kampeni zake za uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Desemba 20. Hili ni tukio la kwanza kubwa tangu kuanza kwa kampeni hii ya uchaguzi ambayo inafanyika katika hali ya mvutano wa kisiasa.

Mgombea urais nchini DRC, Moïse Katumbi, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Beni huko Kivu Kaskazini, Novemba 26, 2023.
Mgombea urais nchini DRC, Moïse Katumbi, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Beni huko Kivu Kaskazini, Novemba 26, 2023. © ARLETTE BASHIZI / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Kinshasa, Pascal Mulegwa

Hali ya mvutano iliripotiwa kabla ya kutua kwa ndege ya Moïse Katumbi, mamlaka ilimkataza mpinzani huyo kufanya katika eneo maarufu kwenye barabara mkuu ya mji wa Kindu.

Alipowasili, Moïse Katumbi na washirika wake, akiwemo Waziri Mkuu wa zamani Matata Ponyo na Seth Kikuni, walishangiliwa na kufuatwa na umati wa watu mitaani kabla ya mkutano huo kuhamishiwa sehemu nyingine. Ni wakati wa kukaribia makazi ya mkuu wa mkoa ambapo mpinzani huyo na wafuasi wake walishambuliwa kwa kurushiwa mawe na vijana wanaodaiwa kuwa wa chama cha rais.

"Kuawa kwa kupigwa mawe", kulingana na chama chake

Katika mabadilishano hayo na umati wa watu, mkuu wa msafara huo, Dido Kakisingi, kiongozi wa vijana wa chama cha Ensemble pour la République cha Moïse Katumbi huko Kindu, alipigwa na kifaa cha kulipuka. Akiwa chini, alipigwa sana hadi akafa, kulingana na chama chake, kikithibitisha kwamba "alipigwa mawe".

Lakini kwa mujibu wa meya wa Kindu, kada huyo wa Chama cha Moïse Katumbi alianguka kutoka kwenye gari lililokuwa kwenye msafara wa kiongozi huyo kabla ya kugongwa na gari nyingine. Polisi waliingilia kati na kufyatua risasi za moto. Katika hali hiyo, watu kadhaa wameripotiwa.

Matukio haya hayakupunguza kasi ya maandamano ya Moïse Katumbi ambaye alifanya mkutano wake kuomba kura kwa wananchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.