Pata taarifa kuu

Senegal: Macron amteua Macky Sall kuwa mjumbe maalum wa 4P, muungano wa upinzani walaani

Sehemu ya upinzani wa Senegal ilichapisha barua ya wazi Ijumaa jioni iliyoelekezwa kwa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. Katika waraka huu, wanachama wa FITE (Muungano kwa ajili ya ushirikishwaji na uwazi wa uchaguzi), wanapinga kuteuliwa kwa Rais wa Senegal Macky Sall kwa wadhifa wa mjumbe maalum na rais wa kamati ya ufuatiliaji ya Mkataba wa Paris wa sayari na watu (4P). Uteuzi uliotangazwa na mwenzake wa Ufaransa siku chache zilizopita.

Macky Sall aliteuliwa kuwa mjumbe maalum wa Mkataba wa Paris kwa sayari na watu na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Macky Sall aliteuliwa kuwa mjumbe maalum wa Mkataba wa Paris kwa sayari na watu na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron. Β© Pierre RenΓ©-Worms/RFI
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Dakar, Birahim Toure

Uteuzi huu unaonekana na FITE, Muungano kwa ajili ya ushirikishwaji na uwazi wa uchaguzi, kama aibu kwa raia wa Senegal. Kwa mujibu wa viongozi 36 waliotia saini kwenye barua hii, rais wa Ufaransa hapaswi kuharakisha kutoa nafasi hii kwa Rais Macky Sall, ambaye bado hajakamilisha mamlaka yake, hata ikiwa ameamua kutowania muhula mwingine.

FITE inaamini kuwa rais wa Ufaransa aliingilia siasa za ndani za Senegal kwa kumsifu rais wa Senegal na demokrasia nchini humo. Jambo ambalo ni ukosefu wa ufahamu wa ripoti mbalimbali kutoka kwa misheni za uchaguzi zilizotumwa nchini Senegal mwaka 2021 na 2022, kwa mujibu wa upande wa upinzani. Uchunguzi ambao unaibua mapungufu katika michakato ya uchaguzi nchini Senegal.

Wanachama wa upinzani pia wanamkumbusha rais wa Ufaransa juu ya wahasiriwa wengi wa maandamano ya Machi 2021 na Juni 2023. Kulingana na wao, angalau watu 100 waliuawa kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano haya maarufu. Zaidi ya watu elfu moja bado wanazuiliwa katika magereza ya nchi hiyo.

FITE pia imemkumbusha Emmanuel Macron kwamba ni chini ya utawala wa Macky Sall ambapo utawala ulikataa kukabidhi fomu za udhamini kwa mwakilishi wa mgombea wa upinzani licha ya uamuzi wa mahakama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.