Pata taarifa kuu

Liberia: Boakai amemsifu rais George Weah, kwa kukubali kushindwa

Katika hotuba yake ya kwanza kabisa tangu atangazwe mshindi wa uchaguzi wa Liberia, rais mteule Joseph Boakai, amemsifu rais George Weah, kwa kukubali kushindwa baada ya muhula mmoja pekee madarakani.

Makamu huyo wa zamani wa rais, alitangazwa mshindi wa duru ya pili ya uchaguzi wa urais baada ya kupata kura asilimia 50.64
Makamu huyo wa zamani wa rais, alitangazwa mshindi wa duru ya pili ya uchaguzi wa urais baada ya kupata kura asilimia 50.64 REUTERS - CARIELLE DOE
Matangazo ya kibiashara

Aidha aliongeza kuwa, ameunda timu yake ya mpito ambayo itafanya kazi na Serikali ya rais Weah ili kuhakikisha makabidhiano ya ofisi yanafanyika kwa utulivu.

"Nyinyi watu wa Liberia mumezungumza, mumweka imani yenu kwangu ya kuongoza mabadiliko ambayo mnataka na mabadiliko hayo yanaanza sasa hivi." alisema Joseph Boakai.

Makamu huyo wa zamani wa rais, alitangazwa mshindi wa duru ya pili ya uchaguzi wa urais baada ya kupata kura asilimia 50.64 ya kura zote dhidi ya rais anayeondoka madarakani George Weah.

George Weah wakati akikubali matokeo ya uchaguzi alisema raia wa Liberia ndio wameshinda katika uchaguzi huo
George Weah wakati akikubali matokeo ya uchaguzi alisema raia wa Liberia ndio wameshinda katika uchaguzi huo © AFP

Boakai anatarajiwa kushika hatamu ya kuongoza taifa hilo mwezi Januari baada ya muda wake Weah kukamilika.

Katika hotuba yake aliyoitoa katika afisi yake ya kibnafsi katika jiji kuu la Monrovia, Boakai pia aliwashukuru raia wa Liberia kwa kumchagua.

Joseph Nyuma Boakai ameahidi kupambana na tatizo la rushwa
Joseph Nyuma Boakai ameahidi kupambana na tatizo la rushwa AFP/Seyllou

Aidha rais huyo mteule ameapa kupambana na changamoto kubwa kwenye taifa hilo ambayo amesema ni ufisadi haswa kwenye serikali akiahidi pia kuboresha miundombinu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.