Pata taarifa kuu

Kenya: Mafuriko yanaendelea kuripotiwa katika baadhi ya maeneo

Nairobi – Milii ya maofisa wawili wa halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini Kenya, ambao walikuwa wamesombwa na mafuriko wakati wakiwa safarini pwani ya Kenya Ijuma iliyopita, imepatikana hapo jana Jumapili.

Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya linasema kuwa zaidi ya watu elfu 20 wamepoteza makazi yao kutokana na mafuriko
Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya linasema kuwa zaidi ya watu elfu 20 wamepoteza makazi yao kutokana na mafuriko REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wakati huu mamlaka ikithibitisha kuwa watu 10 wamefariki kutokana mafuriko yanayoendelea pwani ya taifa hilo la Afrika Mashariki, mafuriko ambayo yamesababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Kwa mujibu wa kamishena wa polisi katika eneo la pwani ya Kenya, Rhoda Onyancha zaidi ya familia elfu 20 zimepoteza makazi yao katika kaunti za Mombasa, Kilifi, Kwale na Tana River kutokana na mafuriko.

Kaunti ya Mombasa nchini Kenya ni mojawapo ya maeneo yalioathirika zaidi ya mafuriko yanayotokana na mvua inayoendelea kunyesha kwenye taifa hilo
Kaunti ya Mombasa nchini Kenya ni mojawapo ya maeneo yalioathirika zaidi ya mafuriko yanayotokana na mvua inayoendelea kunyesha kwenye taifa hilo REUTERS - STRINGER

Watu kadhaa wamethibitishwa kufariki katika maeneo tofauti ya nchi, wakati maelfu ya wengine wakiripotiwa kupoteza makazi yao tangu kuaanza kwa mvua kubwa mwanzoni mwa mwezi Novemba.

Mvua kubwa pia imeripotiwa kusababisha mafuriko ambayo yamewaua watu kadhaa katika nchi jirani za Somalia na Ethiopia.

Idara ya utabiri wa hali ya anga nchini Kenya imeonya kuwa mvua hiyo itaendelea kunyesha hadi mwezi Januari mwaka ujao
Idara ya utabiri wa hali ya anga nchini Kenya imeonya kuwa mvua hiyo itaendelea kunyesha hadi mwezi Januari mwaka ujao REUTERS - STRINGER

Takwimu za shirika la msalaba mwekundi nchini humo zinaonyesha kuwa zaidi ya watu eflu 58 wameathiriwa na mafuriko hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.