Pata taarifa kuu

Liberia: George Weah akubali kushindwa na Joseph Boakai

Rais wa sasa wa Liberia na mwanasoka wa zamani George Weah amekubali kushindwa na mwanasiasa wa upinzani  Joseph Boakai baada ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais kwenye taifa hilo.

Weah amesema sasa ni wakati wa kuweka masilahi ya taifa kwanza.
Weah amesema sasa ni wakati wa kuweka masilahi ya taifa kwanza. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Weah amesema sasa ni wakati wa kuweka masilahi ya taifa kwanza.

Kwa mujibu wa matokeo yay a awali, Boakai alikuwa akiongoza kwa karibia asilimia 51 ya kura kwenye taifa hilo la Afrika.

Katika taarifa yake Weah ameeleza kuwa mpinzani wake anaoongoza kwa idadi ya kura ambazo hawezi mpita.

George Weah-Président sortant du Libéria.
Weah amezungumza na Boakai kumpongeza kwa ushindi wake REUTERS - CARIELLE DOE

Aidha kiongozi huyo anayeondoka madarkani ameeleza kuwa chama chake cha CDC kimepoteza katika uchaguzi huo wa urais japokuwa nchi ya Liberia imeshinda.

Boakai mwenye umri wa miaka 78, alishindwa na Weah mwenye umri mwa miaka 57 kwa asilimia ndogo zaidi ya kura katika uchaguzi wa urais wa mwaka wa 2017.

Kwa mujibu wa matokeo kutoka katika zaidi ya asilimia 99.5 ya vituo vya kupiga kura, Boakai alikuwa amefanikiwa kupata asilimia 50.89 ya kura zilizopigwa kwa mujibu wa tume ya uchaguzi.

Weah na Boakai walishindwa kupata asilimia ya kura hitajika katika duru ya kwanza ilikutangazwa mshindi
Weah na Boakai walishindwa kupata asilimia ya kura hitajika katika duru ya kwanza ilikutangazwa mshindi © Bineta Diagne/RFI

Kulingana na matokeo ya hapo jana Ijumaa, Boakai alikuwa mbele ya Weah kwa kura 28,000.

Katika duru ya kwanza ya uchaguzi, wawili hao hawakuweza kupata kura zilizohitajika kwa mujibu wa katiba ya taifa hilo ilikutangazwa mshindi.

Serikali ya rais Weah imekuwa ikituhumiwa kwa ufisadi pamoja na kiongozi huyo kushindwa kutekeleza ahadi alizotoa kwa raia wake wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.

Kwa mujibu wa matokeo ya hapo jana Ijumaa, Boakai anaoongoza kwa zaidi ya kura elfu 25
Kwa mujibu wa matokeo ya hapo jana Ijumaa, Boakai anaoongoza kwa zaidi ya kura elfu 25 REUTERS - CARIELLE DOE

Marekani imempongeza rais mteule Boakai kuelekea ushindi wake, ikimpongeza pia Weah kwa kukubali matokeo kwa njia ya amani.

Weah pia ameeleza kuwa amezungumza na Boakai na kumpongeza kwa ushindi wake.

Joseph Boakai, ndiye rais mteule wa Liberia.
Joseph Boakai, ndiye rais mteule wa Liberia. © Bineta Diagne / RFI

Weah atasalia kuwa rais hadi mwezi Januari kabla ya kumkabidhi madaraka mrithi wake na ameahidi kuendelea kuwahudumia raia wa Liberia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.